Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wajibu, Ludovick Utouh akizungumza na wadishi wa habari jijini Dar ers Salaam jana.Kushoto ni Afisa mahusiano Hassan Kisena.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa kutowajibika ipasavyo kwenye matatizo yao kutokana na kutokuwepo kwa kiunganishi cha moja kwa moja kati ya wawakilishi na wanaowakilishwa.
Hayo amesema leo Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fikra ya Uwajibikaji Nchini (WIPA), Ludovick Utouh wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kutokana na kiunganishi nchi nyingi zimeingia katika migogoro kati ya wananchi na serikali zao yanayosababishwa na maamuzi ambayo yanaathiri maisha yao.
Amesema kuwa kuwa taasisi hiyo imeanzishwa kwa ajili ya masuala ya uwajibikaji na utawala bora kwa kufungua mlango utakaochochea na kuongeza uelewa mpana wa dhana ya uwajibikaji na utawala bora nchini.
"Kuwezesha Wananchi Kushiriki Kikamilifu Kwenye Masuala ya Uwajibikaji na Utawala Bora Katika Usimamizi wa Rasilimali za Umma" amesema Utouh. Amesema uhamasishajRi wa wananchi kwenye ushiriki katika masuala ya uwajibikaji na utawala bora ni jambo la msingi katika kuhakikisha maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa dhana hii yanakuwa endelevu.
Aidha amesema jitihada za kuimarisha uwajibikaji nchini zilitaachiwa Bunge na taasisi za usimamizi za serikali peke yao, uwezekano wa kufanikisha utekelezaji huu utakuwa ni mdogo kwa sababu suala la uwajibikaji linahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali ili kuleta tija kwa taifa.
Ludovick Utouh Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) – Mstaafu kwa kushirikiana na aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Mafuta nchini ,(TPDC),Yonna Killagane waliona hitaji la kuanzisha Taasisi-Fikra ya Usimamizi isiyo ya kiserikali itakayomilikiwa na wananchi wenyewe ambayo itahusika na uchambuzi wa mfumo na masuala ya uwajibikaji na utawala bora nchini.
Amesema wameandaa mkutano wa kwanza wa kimataifa utakaohusu uwajibikaji katika sekta ya gesi asilia na mafuta kwa kuzingatia umuhimu wa sekta hii kwenye maendeleo ya nchi utakaofanyika kuanzia Aprili 11 hadi 12 Aprili 2016 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere
Amsema wazungumzaji katika mkutano huo ni nchi ambao ni pamoja na, Al Kassim Mtaalam wa mafuta na gesi kutoka Norway, Prof. Patrick Lumumba kutoka Kenya, Bw. Lai Yahya kutoka Nigeria; kwa upande wa Tanzania ni pamoja na Mtendaji Mkuu wa TWAWEZA, Aidan Eyakuze, Dk Abel Kinyondo kutoka REPOA na Prof. Honest Ngowi wa Chuo Kikuu Mzumbe.