Na Abdulaziz Ahmeid, Lindi.
Kilio cha wakazi wa kata ya kitumbikwera na Msinjahili katika Halmashauri ya manispaa ya lindi cha kukosa usafiri wa uhakika kimepata ufumbuzi baada ya kupatiwa boti na Halmashauri hiyo aina ya faiba ambayo hadi Uzinduzi Imegharimu shilingi Milioni 44 zilizotokana na mapato ya Manispaa hiyo.
Akisoma taarifa fupi kabla ya uzinduzi wa boti hilo mkurugenzi wa manispaa ya lindi ndugu Jomaary Mrisho Satura alisema lengo kubwa la Halmashauri hiyo kununua boti ni moja ya Njia ya kurahisisha Utoaji wa Huduma kwa jamii zilizo katika kata zilizo Upande wa pili wa bahari ya Hindi katika manispaa hivyo kwa kutambua kero hiyo wameona umuhimu wa kuwapatia usafiri wa uhakika.
"maeneo yale wapo wanafunzi watumishi mbalimbali ambao wanahitaji huduma hii lakini pia kuna zahanati ambapo kunawakati mwingine kunakuwa na wagonjwa wanaopewa Rufaa ambao wanatakiwa kufikishwa hospital ya rufaa ya Sokoine kwa haraka zaidi isitoshe itasaidia watumishi na wanafunzi kuwahi"alimalizia Satura.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo ndugu Frank Magali ameishukuru Halmashauri na baraza la Madiwani kwa kupitisha Ununuzi wa boti hiyo licha ya kutoa huduma pia ni moja ya chanzo kizuri cha mapato kwa manispaa yetu huku Tukisubiri Utekelezaji wa Ahadi ya Mhe Rais kutununulia pantoni ili kuharakisha maendeleo na hii inawapa faraja kuona tozo na kodi mbalimbali za Halmashauri zinarudi kwa wananchi kwa kuwahudumia....Alimalizia Magali.
Akizindua boti hiyo mkuu wa wilaya ya lindi,Yahya Nawanda alisema kuwa boti hiyo ni kwa ajili ya wakazi wa lindi na hasa wa manspaa na kuonyesha Umuhimu wa utoaji wa huduma na kusaidia Jamii,Nawanda ametoa Fursa kwa wanafunzi,Akina mama wajawazito,wagonjwa wenye Mahitaji maalum pamoja na watumishi wa serikali watakuwa wanavuka bure kwa kutumia Boti hiyo.
Nae bi zahara selemani Ambae ni Diwani wa Kata ya Mikumbi katika manispaa hiyo alisema ni faraja kuona Halmashauri imetambua changamoto inayowakabili Wakazi wa maeneo hayo na kuwapatia boti kwa sababu usafiri kwa kuwa ni muhimu sana ukizingatia hii ni bahari na vinatakiwa vyombo vya usafiri Vinavyomilikiwa na Halmshauri kwa ajili ya kusaidia huduma muhimu kwa wakati wote.
Boti iliyonunuliwa na Manispaa ya Lindi kwa ajili ya Utoaji huduma na kuongeza mapato ya halmashauri.
Muundo wa ndani wa boti hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 40.
Wanafunzi wakiteta na mkuu wa wilaya wakati akifanya uzinduzi wa boti hiyo ikiwemo kumshukuru kwa kuagiza wanafunzi wapande Boti hiyo Bila malipo.
Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Yahya Nawanda akishuka kutoka katika boti hio baada ya kuizindua ili kutoa huduma za usafiri. Boti hiyo imenunuliwa kwa mapato ya ndani ya Halmshauri.