| Maofisa kutoka Serikali ya Japan. | 
| Mazungumzo yanaendelea. | 
| Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akikabidhi zawadi ya picha kwa Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Japan. | 
| Balozi Mahiga akiagana na Mgeni wake. | 
TAARIFA                    FUPI YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA                    AFRIKA MASHARIKI, KIKANDA NA KIMATAIFA KUHUSU UHUSIANO                    KATI YA JAPAN NA TANZANIA TAREHE 15 DESEMBA 2015
           Waziri wa Mambo ya Nje                        na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na                        Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga                        amefanya mazungumzo leo na Waziri wa Nchi wa Mambo                        ya Nje wa Japan, Mhe. Seiji Kihara ambaye                        aliwasili nchini jana kama Mjumbe Maalum wa Waziri                        Mkuu wa Japan Mhe. Shinzo Abe ambapo kesho tarehe                        16 Desemba 2015 anatarajiwa kuwasilisha Ujumbe wa                        Waziri Mkuu wa Japan kwa Rais wa Jamhuri ya                        Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John                        Pombe Joseph Magufuli.  
          Pamoja na                        kuwasilisha ujumbe kwa Mheshimiwa Rais, mgeni huyo                        anatarajiwa kuhudhuria hafla ya utiaji saini wa                        mkataba wa mkopo wa dola za kimarekani milioni 96                      utakaotolewa                        na Serikali ya Japan kwa ajili ya mradi wa                        ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme wa Kenya na                        Tanzania wenye urefu wa kilometa 441.5 kutoka                        Singida na Manyara kupitia Babati na Arusha mpaka                        Namanga. 
            MAHUSIANO KATI YA                      TANZANIA NA JAPAN
          Tanzania na Japan                        zimekuwa katika uhusiano na ushirikiano wa karibu                        mara tu baada ya Tanzania kupata uhuru wake.                        Mahusiano hayo yamekuwa yakikua na kuimarika miaka                        hadi miaka katika nyanja mbalimbali ikiwemo                        miundombinu, afya, nishati, Kilimo, biashara,                        viwanda, usafirishaji na uwekezaji. Kufanyika kwa                        ziara hii ya Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa                        Japan ni muendelezo wa kukuza ushirikiano baina ya                        nchi zetu mbili. 
            MIRADI MIPYA                      ITAKAYOFADHILIWA NA SERIKALI YA JAPAN
           Serikali imeingia makubaliano                        na Serikali ya Japan kutekeleza miradi mitatu ya                        ujenzi wa barabara yenye lengo la kupunguza tatizo                        la msongamano wa magari jijini Dar es Salaam                        linaloathiri uchumi wa nchi yetu. Miradi hiyo ni                        pamoja na:
           Mradi wa Ujenzi wa                      Barabara ya Juu katika eneo la TAZARA (TAZARA                      flyover): 
           Mkataba wa ujenzi wa                        Barabara hiyo tayari ulikwishasainiwa tangu tarehe                        15 Oktoba 2015 na ujenzi unategemewa kuanza mapema                        mwakani.
            Mradi ya Ujenzi wa                      Barabara ya Morocco – Mwenge
           Serikali ya Japan itafadhili                        upanuzi wa barabara ya Mwenge – Morocco ili kuweza                        kupunguza msongamano wa magari. Upanuzi wa                        barabara hii nao unatarajiwa kuanza mwakani.                        Tayari Serikali imekwishaanza hatua za mwanzo za                        ujenzi wa barabara hiyo kufuatia uamuzi wa Mhe.                        Rais kuelekeza fedha zilizokuwa zigharamie sherehe                        za uhuru zitumike kuanza kazi ya upanuzi wa                        barabara hiyo.
            Mradi wa Ujenzi wa                        Barabara ya Gerezani mpaka bendera tatu 
                    Mradi huu unatarajiwa                        kutekelezwa kwa fedha za msaada kutoka Serikali ya                        Japan. Ujenzi wa barabara hii nao unatarajiwa                        kuanza mwakani.
          Mbali na miradi ya ujenzi wa                        barabara, Serikali ya Japan imeingia makubaliano                        na Serikali ya Tanzania kutekeleza miradi ya umeme                        kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa umeme wa                        kutosha kwa matumizi ya wananchi na viwandani kama                        ilivyoahidiwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM.                        Miradi itakayotekelezwa kwa ufadhili kutoka Japan                        ni pamoja na:
           Mradi ya Ujenzi wa Njia                      ya Kusafirishia Umeme Kenya – Tanzania Power                      Interconnection Project
           Mradi huu una lengo la                        kuimarisha usambazaji kwa kuuza na kununua umeme                        katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa                        Kenya. Ni ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme                        wenye KV400 na urefu wa kilomita 414.5 kutoka                        Singida na Namanga kupitia Babati na Arusha.
          Mkataba wa mradi huu                        unatarajiwa kutiwa saini baadaye leo Wizara ya                        Fedha na kushuhudiwa na Waziri wa Nchi wa Mambo ya                        Nje wa Japan.
           Ujenzi wa mradi wa Mtambo                      wa kuzalisha umeme katika eneo la Kinyerezi                      (Kinyerezi II power plant project). 
           Mkataba wa ujenzi wa Mitambo                        ya kuzalisha umeme wa MW 300 huko Kinyerezi                        ulisainiwa tarehe 27 Machi 2015 kati ya Serikali                        na Benki ya Kimataifa ya Ushirikiano wa                        Kimaendeleo ya Japan (Japan Bank for International                        Cooperation – JBIC). Utekelezaji wa Mradi huu                        unatarajiwa kuanza mapema mwakani.
           
