Mkurugenzi Mtendaji wa                Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(watatu toka kushoto)akiwa                ameshikana mikono na baadhi ya viongozi wa taasisi                zilizowezeshwa na Kampuni hiyo kufanya wanajamii maisha                yao kuwa murua.Wakati wa hafla ya Uzinduzi wa kampeni mpya                ya kampeni hiyo ya"Life is better" inayolenga kuendelea                kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi kwa                kutuma na kupokea pesa kwa M PESA kwa haraka na salama                zaidi,Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.Kutoka                kushoto katika picha Msimamizi wa kituo cha Mabinti                Centre,Katia Geurts,Mmoja wa akina mama aliyepona Fistula                Cherry Msangi,Mkurugenzi wa walemavu katika Hospitali ya                CCBRT,Brenda Msangi na Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus                Rwehikiza. 
                Mkurugenzi Mtendaji wa                Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kushoto)akijadiliana jambo na                Mkurugenzi wa walemavu wa hospitali ya CCBRT,Brenda Msangi                wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni mpya ya kampeni                hiyo "Life is better" inayolenga kuendelea kunufaisha                jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi na kutuma na                kupokea pesa kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi                ,Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam. 
                Mmoja wa akina mama                aliyetibiwa na kupona Fistula katika hospitali ya CCBRT,                Cherry Msangi akitoa ushuhuda kwa waandishi wa habari                wakati wa Uzinduzi wa kampeni mpya ya Vodacom Tanzania ya"                Life is better" inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa                kutoa intanet yenye kasi zaidi na kutuma na kupokea pesa                kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi,Uzinduzi huo                ulifanyika jijini Dar es Salaam,Wengine katika picha ni                Msimamizi wa kituo cha Mabinti Centre,Katia Geurts na                Mkurugenzi wa walemavu katika Hospitali ya CCBRT,Brenda                Msangi(kulia). 
                Mkurugenzi Mtendaji wa                Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akiongea na waandishi wa                habari pamoja na wadau mbalimbali(hawapo pichani)wakati wa                hafla ya Uzinduzi wa kampeni mpya ya kampuni hiyo ya "Life                is better inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa                intanet yenye kasi zaidi na kutuma na kupokea pesa kwa                M-PESA kwa haraka na salama zaidi,Uzinduzi huo ulifanyika                jijini Dar es Salaam. 
                Baadhi ya waandishi wa                habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom                Tanzania, Ian Ferrao(hayupo pichani)wakati wa hafla ya                Uzinduzi wa kampeni mpya ya kampuni hiyo ya "Life is                better inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa                intanet yenye kasi zaidi na kutuma na kupokea pesa kwa                M-PESA kwa haraka na salama zaidi ,Uzinduzi huo ulifanyika                jijini Dar es Salaam. 
        Mkurugenzi Mkuu wa                Vodacom Tanzania,Ian Ferrao amezindua kampeni mpya ya                 kampuni hiyo inayojulikana Kama 'Life is Better,'katika                hafla iliyofanyika jijini Dar esk Salaam.Kampeni hii                inadhihirisha ni kwa jinsi gani Vodacom imeweza kuleta                mabadiliko kwenye jamii ya watanzania tangu ianze kutoa                huduma nchini, pamoja na mafanikio hayo  mwaka 2016                imejizatiti kuendelea kuleta mabadiliko makubwa kwa                kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa sayansi na                teknolojia,"alisema Ferrao na kuongeza kuwa kampuni                inajivunia kutoa huduma za maongezi na intanet yenye kasi                kubwa ambazo zinawezesha wateja kuzitumia kubadilisha                maisha yao na kubuni fursa mpya.
        Ikiwa ni kampuni                inayoongoza kwa kuwa na mtandao mkubwa nchini mwaka wa                2015 imepata mafanikio makubwa kwa kuanzisha huduma                mbalimbali  ambazo zimegusa maisha ya watanzania wengi                katika kuzitumia na zinazidi kuwarahishia maisha na                zimewawezesha kuingia katika ulimwengu wa  teknolojia.
        "Mwaka huu umekuwa wa                mafanikio makubwa ambapo Vodacom imeweza kubuni huduma  za                kuboresha maisha ya wateja wetu kupitia mawasiliano na hii                imetokana na mkakati wa kampuni wa kuwekeza katika                miundombinu  ya mawasiliano,wafanyakazi wake na kwenye                ubunifu wa kiteknolojia na ndio maana  imeweza kuanzisha                huduma mbalimbali  za kuwarahisishia maisha wateja wake                ambazo wanaendelea kuzifurahia".Alisema
        Hadi sasa, Vodacom                imewekeza dola za Marekani bilioni moja, na imejenga                mtandao wa kutoa huduma za intaneti za 2G na 3G                unaowafikia asilimia 87 ya Watanzania nchini kote na                imeongeza idadi ya wateja wake  kufikia ziadi ya milioni                12.
        Alisema mwaka wa 2015                ulianza kwa Vodacom kuanzisha promosheni kubwa ya                JayMillions  iliyokuwa inatoa  nafasi ya washiriki                kujishindia hadi shilingi milioni 100 kwa siku na wateja                walioshiriki na kushinda maisha yao yamebadilika na kuwa                bora na kufanikiwa kutimiza ndoto  zao .
        "Promosheni ya                JayMillions imebadilisha maisha ya washindi kwa ndoto zao                kutimia,wapo ambao wameendeleza biashara zao,wapo ambao                wamejiendeleza kielimu,wao waliojenga nyumba na kuanzisha                biashara.Tunajivunia kushiriki katika hatua ya kubadilisha                maisha yao kutokana na zawadi za fedha walizojishindia                kupitia promosheni hii."Alisema Ferrao.
        Mafanikio mengine ya                kampuni aliyabainisha kuwa ni kuzidi kukua kwa Huduma ya                M-Pesa inayotumiwa na watanzania  zaidi ya wateja  milioni                7 nchini na ikiwa na mtandao wa mawakala zaidi ya 85,000                nchini kote imevuka mipaka ya nchi kwa ushirikiano na                Kampuni za Safaricom ya Kenya na MoneyGram  ambapo hivi                sasa mteja anaweza kutuma na kupokea fedha kutoka nje ya                nchi kupitia huduma hii,vilevile huduma ya kujiwekea akiba                na kukopa kwa urahisi kupitia simu ya mkononi ya M-Pawa                imezidi kuimarika,kuaminiwa na kutumiwa na wateja wengi. 
        "Zaidi ya wateja milioni                1.5 wanatumia  huduma hii wakiwa wameweka akiba                inayofikiashilingi bilioni 6.8 na mikopo inayofikia                milioni 500 inatolewa kwa wateja,huduma imechangia                kuwezesha watanzania wengi kuweza kupata huduma za                kibenki".Alisema.
        Huduma zinginezo ambazo                zimeanzishwa na kuendelea kufurahiwa na watumiaji wake                baadhi yake alizitaja kuwa ni kampeni ya RED,Spend and                Get.Huduma ya RED inawarahishia maisha wateja wenye                shughuli nyingi ambapo wanapata kifurushi maalumu na                kupata huduma zote za mawasiliano kwa gharama nafuu na                M-Pesa wakati huo huo  wanajipatia ofa ya kurejeshewa                 asilimia 10%kupitia akaunti zao za M-Pesa.
        Vilevile alizitaja                huduma za kuleta furaha na burudani kwa wateja  kama vile                Ishi Kistaa na Mziiki ambazo zinawawezesha wateja                kusikiliza muziki kutoka kwa  wasanii mbalimbali kupitia                simu zao za mkononi  na kuhusu michezo  kampuni inaendelea                kuwa mdhamini wa ligi  ya soka nchini.
        Pia aliitaja huduma ya                Kilimo Klub ambayo imelenga kuboresha maisha ya wakulima                na kuongeza uzalishaji ambapo wakulima wengi hususani                wanaoishi vijijini wanaendelea  kuifurahia kwa kuweza                kupata mikopo yenye masharti nafuu ya M-Pawa ambayo hasa                imewalenga wao ikiwemo kupata taarifa za hali ya hewa na                bei za mazao kwenye masoko. "Vodacom itaendelea kufanya                ubunifu wa  huduma za aina mbalimbali ambazo                zitawarahishia maisha zaidi na kuwafikia watumiaji wengi                wa simu za  mkononi tofauti na sasa ambapo wapo baadhi                hawazipati".Alisema
        Vilevile alibainisha                kazi kubwa iliyofaywa na taasisi ya kuhdumia masuala ya                kijamii ya Vodacom Foundation katika  kuleta mabadiliko                kwenye jamii ambapo kwa mwaka huu ilijikita zaidi kutoa                misaada mbalimbali kwa jamii  nchini kote hususani  kwa                upande wa elimu , afya  na makundi mbalimbali yenye                mahitaji.
        Mwaka huu imewezesha                operesheni kwa ajili ya wanawake 1,000 walioathirika na                fistula, kuwezesha wasichana  kubaki shuleni kupitia mradi                wa Hakuna Wasichoweza  ,kusaidia wahanga wa ugonjwa Sickle                Cell,Saratani,huduma ya uzazi kwa akina mama ya 'Wazazi                Nipendeni,kuendesha kampeni za Usalama barabarani na                kuwezesha zaidi ya wanafunzi  kusoma elimu ya kompyuta kwa                vitendo mashuleni,kufadhili kituo cha MABINTI kinachotoa                mafunzo kwa wanawake waliopona ugonjwa wa Fistula "Dhamira                yetu kubwa ni kuona tunatokomeza ugonjwa wa Fistula nchini                na kukabuliana na changamoto mbalmbali zilizopo katika                sekta ya afya na elimu".Alisema. 
        Mwaka huu  umekuwa wa                mafanikio na Vodacom imeweza  kubadilisha maisha ya maelfu                ya watanzania kuwa bora na imejizatiti na kujipanga                 kupitia kampeni hii ya Life is Better kuendelea kufanya                vizuri mwakani lengo kubwa likiwa ni kutimiza dhamira yake                ya kubadilisha maisha ya watanzania kupitia teknolojia na                kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa sayansi na                teknolojia.
        Katika mwaka ujao                itaendelea kubuni huduma mbalimbali za kuboresha maisha ya                watanzania kupitia teknolojia ikiwemo kuwawezesha                watanzania wengi kuunganishwa na  huduma za internet na                kuwadhihirishia jinsi huduma hii ni ya msingi kwa                kubadilisha maisha ya watu na kujenga Tanzania  iliyo bora                katika miaka ijayo.
        




 
