Thursday, December 03, 2015

TAZARA yapokea mabehewa 18 na vichwa 4 kutoka Serikali ya Watu wa China


TAZARA yapokea mabehewa 18 na vichwa 4 kutoka Serikali ya Watu wa China
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka akipanda kwenye moja ya vichwa 4 vya treni ya Tazara vilivyotolewa na Serikali ya China.
Mwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing akizungumza kabla ya makabidhiano.
Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga akizungumzia umuhimu wa reli ya TAZARA kwa Tanzania na Zambia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka akizungumzia mustakbali wa TAZAMA katika kujenga uchumi wa Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) Ronald Phiri, akitia saini mkataba wa makabidhiano.
Makamu wa Rais wa CCECC kutoka Serikali ya Watu wa China Lin Zhiyong akisaini makabidhiano.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) Ronald Phiri akibadilishan hati za makabidhiano ya mabehewa 18 na vichwa 4 vya treni na Makamu wa Rais wa CCECC kutoka Serikali ya Watu wa China Lin Zhiyong.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka (katikati) akikata utepe pamoja na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga (kushoto) na Mwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania, wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa kwa kwa mabehewa 18 na vichwa 4 kutoka Serikali ya China.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga, wakielekea kupanda kwenye treni ya kichwa na mabehewa mapya ya TAZARA.
Moja ya mabehewa mapya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga, wakiteremka kutoka kwenye moja ya behewa jipya baada ya kusafiri nalo kwa dakika kumi kufanyia majaribio.
Moja ya kichwa kipya na mabahewa 18 mapya yaliyokabidhiwa kwa TAZARA.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano.
Baadhi ya maafisa kutoka Serikali ya Watu wa China na wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), wakishuhudia utiaji saini wa makabidhiano ya mabehewa 18 na vichwa 4 kutoka Serikali ya Watu wa China. Picha na Hussein Makame-MAELEZO