Friday, December 04, 2015

MANISPAA YA ILALA WASHIRIKIANA NA FORUMCC KUANZISHA MFUKO WA MAZINGIRA NA MABADILIKO YA TABIANCHI.



MANISPAA YA ILALA WASHIRIKIANA NA FORUMCC KUANZISHA MFUKO WA MAZINGIRA NA MABADILIKO YA TABIANCHI.
MANISPAA  ya Ilala kwa kushirikiana na ForumCC wako katika hatua za mwisho za uanzishaji wa Mfuko wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi ukiwa na lengo la kukusanya pesa za kukabiliana na changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi katika eneo hilo

Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya Ilala, Abdon Mapunda anasema baada ya kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa maoni ya wadau wa mazingira, mfuko huo utaanza mara moja kabla ya mwaka 2015 kumalizika

Wakati Manispaa ya Ilala ikiwa na jukumu la kusimamia uanzishwaji na uendeshaji wa mfuko huo, ForumCC wao wanajukumu la kutoa msaada wa kitaalamu ili kuhakikisha kuwa mfuko huo unafanikiwa na kufikia lengo lililokusudiwa.
Mtaalamu wa Misitu na Mazingira, Kahana Lukumbuzi ambaye alikuwa na jukumu la kutengezeza andiko la uanzishwaji wa mfuko huo, akitoa ufafanuzi wa baadhi ya vipengele vilivyomo kwenye andiko hilo.
Wadau wa mazingira wakifuatilia mkutano huo.
Sehemu ya mapendekezo ya namna Mfuko wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi utakavyokuwa.
Wadau wa mazingira wakifuatilia mkutano huo.
Wadau wa mazingira wakifuatilia mkutano huo.
Picha zote na Tabianchi.