
Rais Barrack Obama wa Marekani, tayari amewasili mjini Nairobi.

Ndege iliyombeba rais obama ilitua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa mbili za usiku. Alipowasili Rais Obama amelakiwa na mweyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akimkaribisha Rais Barrack Obama wa Marekani alipowasiri katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta leo usiku.
mwendo wa saa mbili na robo rais Obama alitua ndege yake. Alipowasili alizungumza kwa muda mfupi na mwenyeji wake rais Kenyatta na kisha kutia saini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka. Obama sasa ameandikisha historia ya kuwa rais wa kwanza wa Marekani, kuzuru Kenya akiwa ofisini. Obama anatarajiwa kufungua mkutano wa sita wa kimataifa kuhusu ujasiri mali katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi.
Baadaye rais huyo atafanya mashauriano na rais Uhuru Kenyatta katika ikulu ya Nairobi. Siku yan Jumapili rais Obama atahutubia mkutano wa wakuu wa mashirika ya kijamii katika chuo kikuu cha Kenyatta kabla ya kuhutubia mkutano mwingine kwa wakenya wote katika uwanja wa Kasakani. 
Ndege iliyombeba rais obama ilitua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa mbili za usiku. Alipowasili Rais Obama amelakiwa na mweyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.


Rais Barrack Obama wa Marekani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili uwanjani hapo




Rais Obama akipokewa na dadake wa kambo bi Auma Obama na hata akamruhusu kusafiri naye ndani ya gari lake rasmi The Beast.

CHANZO: BBC SWAHILI