Tuesday, July 14, 2015

MILIONI 50 KUTOLEWA KWA ATAKAYEFANIKISHA KUKAMATWA KWA MAJAMBAZI WALIYOVAMIA STAKISHARI




MILIONI 50 KUTOLEWA KWA ATAKAYEFANIKISHA KUKAMATWA KWA MAJAMBAZI WALIYOVAMIA STAKISHARI
Muonekano wa Kituo cha Stakishari, Ukonga jijini Dar kilichovamiwa na majambazi.

Askari polisi akidumisha ulinzi kwenye kituo hicho.
JESHI la Polisi nchini leo limetangaza zawadi nono ya shilingi milioni 50 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa majambazi waliovamia Kituo cha Polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga, Dar juzi.
Zawadi hiyo imetangazwa leo jijini Dar na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova kwa niaba ya jeshi hilo.
Majambazi hao walivamia Kituo cha Polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga, Dar juzi usiku na kuua watu saba wakiwemo askari wanne, raia wawili pamoja na jambazi mmoja aliyeuawa na wenzake hao kisha kupora silaha.
(Habari: Gabriel Ng'osha / GPL)