Zimebaki kama wiki mbili hivi ugeni wa White House utue pale Jomo Kenyatta International Airport, Nairobi Kenya kama ambavyo iliahidiwa.
Safari ya kihistoria ya Rais Obama ndani ya Kenya inakaribia, huu ni uthibitisho mwingine kwamba mambo yameiva… Gari za watu wa Usalama tayari zimeshushwa Nairobi na pia kuna Helicopter zaidi ya nane za Kijeshi tayari zimetua.
Mbali na gari hizo pamoja na helicopter zilizotua, wako Maofisa Usalama zaidi ya 200 ambao tayari wako Kenya kwa ajili ya kuhakikisha mpaka siku Rais Obama anatua kunakuwa na usalama wa kutosha.
Stori nyingine kutoka Nairobi inaonesha timu ya watu wa Usalama watakuwa kama 800 hivi kutoka Marekani na Polisi zaidi ya 2,000 wa Kenya watahusika na Ulinzi wa msafara wa Obama akiwa Kenya.