Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kufua umeme ya TANASI, William Crawford (mwenye tai ya blue), akimtambulisha mjukuu kwake Colin Machamsoc kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, mara baada ya kuwasilia Wizarani hapo walipotembelea Leo Asubuhi kutaka kufahamu fursa zilizo za uwekezaji katika Wizara ya Uchukuzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, akisisitiza jambo kwa kundi la wawekezaji kutoka nchini Marekani waliotembelea Wizara hiyo leo asubuhi, kutaka kufahamu fursa za uwekezaji katika taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi, wawekezaji hao wameonyesha nia ya kuwekeza katika miradi ya Viwanja vya Ndege, Bandari pamoja na reli.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathimini wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. Aunyisa Meena, akiwasilisha mada kwenye mkutano wa uliowakutanisha wawezekezaji kutoka nchini Marekani waliotembelea Wizara ya Uchukuzi leo asubuhi kutaka kufahamu fursa za uwekezaji zilizo katika sekta ya Uchukuzi.
Robert Shumake kutoka Kampuni ya Shukame Rails akikabidhi mchoro wa Treni za mwendo kasi Diesel Multiple Unit (DMU) ambazo inataka kuwekeza katika sekta ya Reli kwa Dkt. Shaaban Mwinjaka, wakati alipomtembelea Wizarani kwa ajiili ya kuangalia fursa za kuwekeza katika sekta ya Uchukuzi. Kampuni hiyo iko kwenye hatua za mwisho za kusaini Memorandum of Understanding (MoU) na Shirika la Reli Tanzania (TRL), kwa ajili ya kutengeneza treni hizo zitakazosafirisha abiria kati ya 800 mpaka 1000.
Afisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), Bw. Ntandu Mathayo (mwenye shati jeupe), akiwaonyesha wawekezaji kutoka nchini Marekani, gati namba 1 mpaka 7 inapoanzia katika bandari ya Dar es Salaam leo asubuhi wakati wawekezaji hao walipotembelea bandari ya Dar es Salaam kuangaliza fursa za uwekezaji katika bandari ziizoko.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Miundombinu wa Mamlaka ya Usimamizi wa BAndari Tanzania, Mhandisi Alois MAtei, akiwaonyesha wawekezaji kutoka nchini Marekani, eneo la Bandari ya Dar es Salaam, leo asubuhi walipotembelea Bandari ya Dar es Salaam kuona fursa za kuwekeza katika sekta ya Uchukuzi.