Afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Bw Jimmy Kiwelu (kulia) akiwa na wafanyakazi wenzake baada ya kutwaa tuzo ya ubora ya Kitaifa katika bidhaa za Asas Dairies Ltd
Hii ndio kampuni iliyoweza kushinda tuzo ya ubora
Medali ,vyeti na tuzo ya ushindi ambayo kampuni ya Asas Dairies Ltd imeshinda tena mwaka huu katika maonyesho ya maziwa mkoani Mara
Vyeti na medali tatu ambazo kampuni ya Asas Dairies Ltd imeshinda tena kwa
Baadhi ya bidhaa za kampuni ya Asas Dairies Ltd zilizoshinda medali
Na Matukiodaima Blog
BIDHAA na maziwa yanayotengenezwa na kampuni ya Asas Dairies Ltd ya mkoani Iringa kwa mwaka wa tatu mfululizo zimeendelea kushikilia tuzo ya ubora na kuwa kampuni bora kuliko makapuni mengine ya maziwa hapa nchini .
Kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd ambayo ni moja kati ya makampuni ya kizalendo nchini na moja kati ya makampuni yaliyopata kupewa tuzo ya ulipaji kodi mzuri na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imeshinda katika maadhimisho ya wiki ya maziwa mwaka huu tena yaliyofanyika wilaya Babati mkoani Mara kwa kushindanisha kampuni zaidi ya 20.
Akizungumzia ushindi huo afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Bw Jimmy Kiwelu alisema kuwa mbali ya kampuni hiyo kuongoza kwa mwaka huu wa tatu mfululizo bado bidhaa zake nyingine zimeendelea kushinda medali mbali mbali na kuonyesha uwezo mkubwa wa kampuni hiyo katika ubora.
Alisema baadhi ya makampuni makubwa ambayo yalipata kuingia katika mashindano hayo ni pamoja na Tanga Fresh, DarFresh,Kilimanjaro Fresh,Creamer Fresh,Cefa, Grand DeMom ya Engingteng, Nansinya ya Arusha ,Nnronga ya Kilimanjaro mengine mengi.
Alisema kuwa bidhaa kwa mwaka huu kila kampuni lilikuwa likishindanisha bidhaa zake tatu huku kampuni yake Asas Dairies Ltd bidhaa zake zote tatu zilishinda na kupewa medali.
Pamoja na kushinda katika bidhaa hizo bado kampuni hiyo ilinyakua tuzo ya jumla katika ubora.
Bw Kiwelu aliwataka watanzania kuendelea kuzipenda bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na kuendelea kuongoza katika ubora na kuwa lengo la kampuni hiyo kuendelea kushinda tuzo za ubora
Pia alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na ushirikiano mkubwa wanaombwa kuihamasisha jamii kuendelea kutumia maziwa hayo na bidhaa nyingine za chini ya kampuni ya kizalendo ya Asas Dairies Ltd.
Bw Kiwelu alisema mwaka huu jumla ya Medali 9 zilikuwa zikishindaniwa ila kampuni Asas Dairies Ltd iliweza kuongoza kushinda medali 3 kati ya 9.
Aliyekuwa mgeni rasmi tena kwa mwaka huu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani pamoja na kupongeza mshindi huyo wa jumla na washiriki wengine katika maonyesho hayo bado alitaka makampuni zaidi kuendelea kushiriki maonyesho hayo kwani yanasaidia kutambua changamoto katika utengenezaji wa bidhaa bora .
Pia alieleza kufurahishwa na hatua kubwa ya kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd kwa kuendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo ya ubora wa maziwa nchini na kuwa mbali ya kuwa ni heshima ya kampuni na mkoa wa Iringa ila bado ni heshima kwa Taifa kuona kamapuni ya ndani yanaonyesha ufanisi mkubwa katika bidhaa zake .