
Zitto alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama hicho nafasi ambayo kwa katiba ya chama hicho ndiyo ya juu zaidi. Nafasi zingine ni Mwenyekiti wa chama, namakamu wake, wa Tanzania visiwani na Tanzania bara, hali kadhalika nafasi ya ukatibu mkuu na manaibu wake wiwili.
Chama hicho kitazinduliwa rasmi Jumapili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Hall jijini Dar es Salaam.
Zitto akionyesha alama ya chama ambayo ni "Uwazi".
Wajumbe wakipiga kura.
Aliyekuwa katibu mkuu wa muda wa ACT-Tanzania, Samson Mwigamba, akihutubia.
Msimamizi wa uchaguzi huo, Profesa Kitila Mkumbo.