Sunday, March 29, 2015

FAST JET KUSAFIRISHA MADAKTARI BINGWA BURE KWENDA KUSAIDIA JAMII ISIYOJIWEZA



FAST JET KUSAFIRISHA MADAKTARI BINGWA BURE KWENDA KUSAIDIA JAMII ISIYOJIWEZA
Kampuni ya Fastjet lipo mbioni kutoa tiketi kwa madaktari bingwa kwenda mikoa inayokwenda kuwapatia huduma ya matibabu ilikuweza kupunguza gharama za nauli kwa wananchi kufika sehemu mbalimbali kupata matibabu hiyo ikiwa ni kurudisha kile kidogo wananchopata kwa jamii.


Hayo yamebainishwa na meneja mkuu Fastjet Afrika mashariki Jimmy Kibati wakati wa kutambulisha safari zake mpya zitakazo anza mwishoni mwa mwezi huu ikiwa ni pamoja na kuzdi kupunguza bei kwa wateja wake wanaosafiri kwa ndege za shirika hilo.

Kibati alisema kuwa katika kuisaidia jamii wameshawasafirisha kwa kutoa tiketi bure kwa madaktari sita wa meno kwenda mkoani Shinyanga kutoa huduma na wakati wowote wapo mbioni mwishoni mwa mwezi kuwapeleka madaktari bingwa sehemu mbalimbali kuweza kutoa huduma ambazo wananchi wasiojiweza wangezifuata Mkoani Dar es salaam hivyo kuzipata mkoani kwake.

Alitanabaisha kuwa shirika hilo la ndege limekuwa na kawaida hiyo tokea lilipoanzishwa miaka miwili iliyopita kwa kutoa misaada kwa jamii isiyojiweza wakiwemo yatima na wajane kote nchini.
"Hapa tunatambulisha kuanza kwa safari za ndege zetu kutoka Kilimanjaro kwenda Mwanza,ambayo itakuwa kwa bei ya 35,000 na safari ya kutoka Kilimanjaro kwenda Entebe nchini Uganda kwa bei ya 95000 na safari hizi zitaanza mwishoni mwa mwezi huu"alisema Kibati.
Alisema kuwa watoa safari tatu kwa wiki kuanzia Jumanne,Alhamisi na Jumamosi kwa kwenda Enteber na itafungua fursa kwa wafanyabishara pia safari ya Kilimanjaro na Mwanza itakuwa mara nne kwa wiki na kuwataka wananchi kusafiri kwa ndege hizo na kufurahia huduma zao