Saturday, March 21, 2015

Vurugu zaendelea kutikisa Tunduma


Vurugu zaendelea kutikisa Tunduma

kikosi cha Zimamoto limevunjwa vioo na askari wa kikosi hicho kujeruhiwa hii leo baada ya kutupiwa mawe na wananchi katika vurugu zinazoendelea kwa siku ya tatu huko Tunduma Mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Ahmed Msangi

Akiongea na East Africa Radio kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mbeya ACP, Ahmed Msangi amesema vurugu hizo zimetokana na mgogoro wa kiwanja baina ya chama cha Mapinduzi CCM na wananchi ambao wamekuwa waking'ang'ania kumiliki kiwanja hicho licha ya maamuzi ya mahakama kutaja CCM ndio mmiliki halali wa kiwanja hicho.

Amesema vurugu hizo ambazo zimesimamisha shughuli zote biashara na kukwamisha pia usafiri katika barabara kuu ya Tunduma, zilianza siku ya jumatatu baada ya wananchi kuhamasishwa na kuvamia uwanja huo na kuanza shughuli za ujenzi wa Zahanati pamoja na Kituo cha polisi, ambapo polisi waliingilia kati na kuwazuia.

Kamanda Msangi amesema watu 26 walikamatwa siku ya Jumatatu katika vurugu hizo ambazo zilisambaa katika barabara kuu na kusababisha barabara kufungwa kwa kuwekwa mawe ambapo pia gari moja la polisi lilivunjwa vioo

Amesema baada ya jana hali kutulia kidogo leo tena vurugu hizo ziliibuka baada ya wananchi kukutana na mbunge wa eneo hilo kupitia Chadema Mhe. David Silinde ambapo wananchi walirejea tena kufanya vurugu mitaani na kufunga barabara kwa mawe na kuchomamoto matairi ya gari, hata hivyo polisi walituliza hali hiyo.