Wednesday, March 25, 2015

Kwa hili lazima Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) mdharauliwe milele



Kwa hili lazima Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) mdharauliwe milele

Udom

Huwa nina mashaka sana na chuo kikuu cha Dodoma, hasa wanafunzi wa chuo hicho, hii ni kwa sababu ya mambo ambayo wanafanya wanafunzi hao.

Ni juzijuzi tuu tulisikia wanafunzi (wasomi wa UDOM) hao watoa tamko la kupinga kuwa bunge kupeleka mapendekezo ya kuwavua uongozi na kuwawajibisha waliohusika na sakata la escrow, jana wameandamana hadi kwa waziri mstaafu aliyeihujumu nchi hii katika kashfa ya Richmond. Nimesikitishwa sana.

Ivi mwanafunzi ambaye unachukua bachelor unaandamana kisa tuu mtu agombee uraisi, najiuliza huo muda mnaupata wapi, tutaweza vipi kuwatofautisha ninyi na ambao hawajasoma? au matejaa? Kwa kweli mnatudhalilisha hata wanafunzi wa vyuo vingine kuwa ni rahisi kufanya upuuzi.

Najiuliza kwanini mambo haya yasifanyike vyuo vinginee kama UDSM, SUA, MZUMBE, MUHIMBILI, KCMC, ST. JOSEPH. Kidogo mnanipa mashaka kweli wanafunzi wanaochaguliwa UDOM na viwango vya ufaulu wenu form 6, mnajidhalilisha sana.

Wakati mwingine mnapoona watu wanadharau chuo chenu msidhani wanafanya makusudi, bali hayo mnayoyafanya ndio sababu, mnapaswa kujua huu ndio wakati wa kukinyanyua chuo chenu kwa kutoa tafiti na sio kufanya mambo ya kipuuzi, mnapaswa kujiheshimu na kuheshimu taaluma zenu.

Mwanachuo hupaswi kujishusha kiasi hicho kama mswahili asiye na majukumu, mnatuaibisha bhana, acheni njaa.