Thursday, February 26, 2015

Watu 2 mkoani singida wamekufa na wengine 29 wamejeruhiwa katika ajali mbili zilizo husisha basi na lori



Watu 2 mkoani singida wamekufa na wengine 29 wamejeruhiwa katika ajali mbili zilizo husisha basi na lori
Watu wawili mkoani Singida wamekufa na wengine zaidi ya ishirini na tano wamejeruhiwa kwa kuvunjika mikono na miguu katika ajali mbili tofauti  zilizo husisha basi na lori na nyingine mwendesha pikipiki  kugongwa na lori.

Akieleza kamanda wa polisi mkoani Singida ACP Thobiasi Sedoyeka amethibitisha kutokea kwa ajali hizo ambazo zimehusisha basi la Ngumuo lenye usajili wa namba T 476 CSH aina ya yutong lilikuwa likitokea Moshi na kuelekea Kahama na lori namba T 343 DCP lenye tela namaba T 936 DBY lilokuwa likitokea mwanza na kuelekea Dar-es-Salaam na kusema kuwa zimesababishwa na mwendokasi wa dereva wa basi na uzembe wakati akiendesha.
Wakielezea jinsi ajali ilivyo tokea majeruhi wamesema dereva wa basi lao alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi huku mvua ikinyesha na gafla wakaona basi lao lina yumba na kugongwa na tela la lori kisha likapunduka mara tatu.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Daktali Daniel Tarimo amesema wamepokea maiti mbili na majeruhi ishirini na sita ambao wamesha patiwa matibabu na wengine itabidi wapewe rufaa ya kwenda hospitali KCMC na Muhimbili kwa sababu wamevunjika vibaya.