Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema jeshi la polisi lilifika katika eneo la tukio nakufanikiwa kuwakamata watu watatu wanasadikiwa kujihusisha na tukio hilo na linaendelea kuwahoji kisha watafikishwa mahakamani.
Aidha kamanda Paulo amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa aliye kimbia ambapo katika hatua nyingine wamefanikiwa kumkamata hawara wa mtu huyo aliyejulikana kwa majina ya Husuna Isimaeli mkazi wa mkindo ambaye alikuwa akimhifadhi mtuhumiwa na jeshi la polisi litaendelea kumshikilia kwa mahojiano ilikumpata mtuhumiwa aliye kimbia.