Monday, February 09, 2015

Maabara zilizojengwa kwa agizo la Rais Kikwete Songea mkoani Ruvuma zageuzwa madarasa ya kusomea




Maabara zilizojengwa kwa agizo la Rais Kikwete Songea mkoani Ruvuma zageuzwa madarasa ya kusomea


 Kutokana na upungufu wa madarasa ya kusomea wanafunzi wa kidato cha  kwanza na cha pili katika shule ya sekondari matarawe iliyoko Songea mkoani Ruvuma  wanasomea  kwenye maabara zilizojengwa kwa agizo la Rais Kikwete na wanalalamikia hatua hiyo kutokana na kuumia kwenye mifereji ya maabara hizo.

Uchunguzi wetu umebaini hilo  na  wanafunzi wamesema kuwa wamekuwa wakisoma kwa shida kwa kuwa vyumba hivyo si rasmi kwa kusomea hivyo wameomba kujengewa madarasa.
 
Diwawani wa kata ya matarawe Bw.James Makene amesema kuwa wameamua kugeuza  maabara kuwa madarasa kwa kuwa hawana madarasa ya kutosha ilhali mwaka huu wamepokea wanafunzi mia mbili wa kidato cha kwanza.
 
Hata hivyo vyumba hivyo vya maabara  awali vilikuwa madarasa  na vimekarabatiwa ili viwe maabara huku ukarabati wake ukilalalamikiwa kwa madai kuwa   uko chini ya kiwango.