Na Chalila Kibuda na Globu ya Jamii ,Dar
Wanafunzi Chimbukizi wa Sayansi wameitaka serikali kuwekeza katika masomo ya sayansi ili nchi kuweza kupata watalaam ambao watasaidia kutatua changamoto katika jamii.
Hayo waliyasema leo wanafunzi wa Sayansi Chimbukizi walioshinda mashindano ya utafiti kwa kutumia malighafi asili ya kutengeneza dawa ya kuua Nzi na Mbuu ambao wamepewa udhamini na Mfuko wa Karimjee Jivanjee (KJF)wa kwenda kusoma nchini Ireland.
Wanafunzi hao ni Dharia Amour Ali na Salma Khalfan Omari kutoka shule ya Sekondari Lumumba iliyopo Unguja Mjini Zanzibar
Mkurugenzi wa Wanasayansi Chipukizi ,Dk.Gosbert Kamugisha alisema wataendelea kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ili nchi kuweza kuwa watafiti wa kisayansi.
Kamugisha alisema utafiti wanasayansi Chipukizi kwa kutafuta dawa ya kuua nzi na mbu kwani dawa ambayo wengi wanaweza kutumia kuliko inayozalishwa na viwanda.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Karimjee Jivanjee (KJF),Hatim Karimjee alisema wamekuwa wakitoa udhamini kwa wanafunzi kwa muda mrefu kwani nia ni kutaka taifa liwe na wataalam watafiti watakaotatua matatizo ya wananchi.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Karimjee Jivanjee (KJF),Hatim Karimjee (wa pili kulia) pamoja na Muwakilishi wa Balozi wa Ireland Tanzania,Carol Hannon wakiwakabidhi Vyeti wanafunzi wawili walioshinda mashindano ya utafiti kwa kutumia malighafi asili ya kutengeneza dawa ya kuua Nzi na Mbuu ambao wamepewa udhamini na Mfuko wa Karimjee Jivanjee (KJF)wa kwenda kusoma nchini Ireland,Wanafunzi hao ni Salma Khalfan Omar (kushoto) na Dhariha Amoor Ali.