Wednesday, January 07, 2015

VIJANA KILIMANJARO WATAKIWA KUSIMAMA IMARA NA KUDAI FURSA MBALIMBALI ZIKIWAMO ZA KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA AJIRA ZINAZOTOKANA NA MLIMA KILIMANJARO


VIJANA KILIMANJARO WATAKIWA KUSIMAMA IMARA NA KUDAI FURSA MBALIMBALI ZIKIWAMO ZA KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA AJIRA ZINAZOTOKANA NA MLIMA KILIMANJARO
VIJANA wa mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kusimama imara na kudai fursa mbalimbali zikiwamo za kupewa kipaumbele katika ajira zinazotokana na mlima Kilimanjaro. 

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini na Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Moshi Vijijini, Innocent Melleck alipokuwa akizungumza na waandishi wahabari juu ya mkakati wa kupambana na wimbi la vijana walio mitaani kwa kukosa ajira katika mkoa wa Kilimanjaro .
  Melleck alisema anatarajia kuitisha mkutano maalum kwa ajili ya kuwakutanisha vijana kujadili namna watakavyoweza kufaidika na fursa zitokanazo na mlima Kilimanjaro hususani katika sekta ya utalii.
Tunatarajia mwishoni mwa mwezi huu kukutanisha vinjana wote wanajishugulisha na shuguli za kupandisha watalii mlimani wakiwepo wabeba mizigo,wapishi na wasimamizi wao ambao ni wazawa ili kuweza kujadili njia sahihi ya kufuata kuweza kushinikiza uongozi wa KINAPA kutoa nafasi kwa vijana wazawa.


Alisema pindi mlima huo ukiwaka moto vyombo vya usalama kutumika kuwakamata wazawa kwenda kuzima moto huo tena kwa kutumia nguvu wakati katika swala la ajira rasmi na zisizo rasmi wazawa wameonekana sii lolote kitu na nafasi kuwewa wageni.

Aliongeza ajira katika mlima Kilimanjaro imeendelea kunuka rushwa na ubaguzi mkubwa jambo ambalo linahita mshikamano wa pamoja kwaaji ya ukombozi wa kizazi cha wazawa wa mkowa wa Kilimanjaro,Aliongeza mkoani Arusha katika mlima meru hakuna mtu ambae sii mmeru anayeweza kupandisha watalii katika mlima huo Zaidi ya wameru jambo ambalo ni kinyume mkoani kilimanjaro

"Lazima vijana wetu wafaidike na fursa hizi za kupata ajira badala ya watu kutoka mikoa mingine kuchukua nafasi hizo na wao kubaki kama watazamaji," Kada huyo wa CCM ambaye ametangaza kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo mwaka huu, alisema unapotokea moto katika mlima huo, vijana ndiyo wanaojitokeza kuuzima hivyo lazima wafaidike nao moja kwa moja.

Alisisitiza kuwa ajira kwa vijana itakuwa ajenga yake namba moja na atahakikisha analipigania hilo kwa nguvu zake zote. "Mlima Kilimanjaro peke yake ukitumiwa vizuri unatosha kutoa ajira za uhakika kwa vijana wetu wa mkoa wa Kilimanjaro hususani jimbo la Vunjo wilaya ya Moshi vijijini ambao kwa sasa hawana ajira," alisisitiza Melleck

Kuhusu uchaguzi mkuu ujao, Melleck alisema amejipanga kulikomboa jimbo la Vunjo ambalo kwa sasa linashikiliwa na Augustino Mrema kupitia Chama cha Tanzania Labour Party (TLP).