Friday, January 23, 2015

Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili katika Chuo cha Ualimu Rukwa Auawa Kinyama




Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili katika Chuo cha Ualimu Rukwa Auawa Kinyama
Mwanafunzi wa ualimu aliyekuwa anasoma mwaka wa Pili katika Chuo cha Ualimu Rukwa, Manispaa ya Sumbawanga, Zakayo Anosisye (25) ameuawa na watu wasiofahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda akithibitisha kutokea kwa mkasa huo alisema kuwa, mwili wa Anosisye uligundulika asubuhi ya Januari 19 mwaka huu katika Kitongoji cha Chanji "B" mjini hapa.
Kamanda huyo amesema kwamba Anosisye ambaye alikuwa anasimamia ukumbi wa kuonesha video ambao ni mali ya ndugu wa karibu naye alikutwa amekufa kwa kupigwa na kitu kizito.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda usiku kabla ya tukio hilo ukumbi huo ulikuwa umefurika idadi kubwa ya watazamaji waliokuwa wakiangalia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Equtorial Guinea ambapo baada ya kumalizika walitawanyika.
Inadaiwa kuwa asubuhi ya siku iliyofuata majirani waligundua mlango wa ukumbi huo ulikuwa umevunjwa na Anosisye akiwa ukumbini mfu kwa kupigwa na kitu kizito kichwani.