Monday, October 06, 2014

SEMINA YA KAMATA FURSA,JITATHIMINI,JIAMINI,JIONGEZE YAFANYIKA MJINI DODOMA



SEMINA YA KAMATA FURSA,JITATHIMINI,JIAMINI,JIONGEZE YAFANYIKA MJINI DODOMA

Mrisho Mpoto akimkabidhi kifaa cha kupimia magari mmoja wa wakazi wa Dodoma Beatrice Chilewa (kulia), muda mfupi baada ya kujishindia moja ya swali lililoulizwa na msemaji wa GS1, Pius Mikongoti, ambalo lilikuwa likimtaka ataje nchi tatu za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazotoa Barcode na namba za utambulisho wa nchi hizo, wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Josekazi Auto Garage ambaye ndiye mmiliki wa kifaa hicho cha kupimia magari.


MKURUGENZI wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba,(wanne kushoto) akiongea na baaddhi ya wakazi wa Dodoma mjini (hawapo pichani) waliohudhuria Semina ya Kamata Fursa ndani ya Ukumbi wa Royal Village mapema jana,ambapo aliwaeleza wakazi hao namna ya kuwapatia mbinu mbalimbali za kujikwamua kupitia rasilimali zilizopo ndani ya mkoa huo wa Dodoma.

Msemaji kutoka GS1, Pius Mikongoti akiwalezea wakzi wa Dodoma namna ya  kunufaika kupitia huduma zitolewazo na GS1, hasa katika mfumo wa kutumia Barcode. 
Msanii wa kughani Mashairi Mrisho Mpoto akiwapa historia yake ya mafanikio na namna alivyoweza kutumia fursa hadi kufikia hapo alipo kwa sasa.

Afisa Utekelezaji na mipango wa NSSF Ally Mkulemba akitoa semina kwa wakazi wa Dodoma, huku akiwapa mbinu za kutumia fursa katika kusongesha mafanikio kupitia mikopo mbalimbali itolewayo na Shirika hilo mapema jana ndani ya Ukumbi wa Royal Village.

Sehemu ya watu waliojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royal Village,mjini Dodoma hapo jana.

PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA