Tuesday, January 06, 2015

Mahiza aagiza wakurugenzi kutofungua sekondari zisizo na vyoo vya walimu na wanafunzi Mkoani lindi



Mahiza aagiza wakurugenzi kutofungua sekondari zisizo na vyoo vya walimu na wanafunzi Mkoani lindi
Na Abdulaziz Lindi,Globu ya Jamii - Lindi

Mkuu wa mkoa wa Lindi,Mwantumu Mahiza amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zilizopo katika mkoa huu wahakikishe shule zote za sekondari ambazo hazina vyoo kwa ajili ya matumizi ya walimu wa shule hizo zijenge kabla hazijafunguliwa.

Mahiza alitoa agizo hilo katika kijiji cha Kilimarondo wilayani Nachingwea katika ziara yake ya siku tatu wilayani Nachingwea.Ambapo alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ujenzi wa maabara kwenye shule za sekondari.

Agizo la mkuu huyo wa mkoa lilitokana na hali aliyoiona katika shule ya sekondari ya kutwa ya Kilimarondo ambayo ina matundu mawili pekee ya vyoo ambavyo ni kwa ajili matumizi ya wanafunzi wa shule hiyo ambayo inatarajia kufunguliwa mwaka huu.

Alisem a nijambo lisilokubalika shule ambazo hazina vyoo zifunguliwe bila kuwa na vyoo,hivyo aliwataka wakurugenzi watendaji kuhakikisha tatizo hilo linashugulikiwa kabla ya muhula wa masomo kuanza.

"naagiza shule ambazo hazina vyoo vya waalimu zisifunguliwe hadi vitapojengwa,nanikatika kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kwani bila kufanya hivyo nikuwadhalilisha na kuwatesa waalimu kitendo ambacho hakikubaliki," alisisitiza Mahiza.Alisema huduma bora kwa waalimu ndizo zitakazo waongeza ari ya kufanya kazi moyo na bidii nakusab matokeo mazuri katika shule wanazofundisha.

Sambamba na agizo hilo,mjuu h uyo wa mkoa amewataka viongozi na watendaji wa serikali katika mkoa huu kuwa karibu na miradi inayojengwa ili waweze kusimamia kikamilifu ujenzi wa miradi hiyo,badala ya kuicha inajengwa bila usimamizi.

Alisema tabia ya kutokuwa karibu na miradi inayojengwa inasababisha ubadhirifu na kujengwa chini ya viwango.Hivyo kuisababishia serikali hasara ambazo zingeweza kuepekwa.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kuhakikisha kwamba zahanati ya kijiji cha Kipara, kata ya Kipara inaanza huduma mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu.