Tuesday, January 06, 2015

KAMPENI YA USALAMA BARABARANI YA" WAIT TO SEND"YAENDELEA KANDA YA ZIWA


KAMPENI YA USALAMA BARABARANI YA" WAIT TO SEND"YAENDELEA KANDA YA ZIWA
Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza 7171 Josephine (kushoto), akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva Alex John wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani humo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya "Wait to Send" inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.
Dereva wa kampuni ya mabasi ya Mohamed Trans, Soud Nassoro (katikati) akitumia kifaa maalum cha kupima kilevi huku askari wa kikosi cha usalama barabara jijini Mwanza, F4278 PC Luge na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa, Domicien Mkama akishuhudia wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika katika kituo cha mabasi Nyegezi Mkoani humo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya "Wait to Send" inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanatumia vyombo hivyo.Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.
Dereva Lucas Kibogi akipuliza kifaa maalum cha kupima kilevi mwilini ili kuangalia kama ana kilevi mwilini wakati wa zoezi maalum la usalama barabarani lililofanyika katika kituo cha mabasi Nyegezi Mkoani humo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya "Wait to Send" inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanatumia vyombo hivyo. Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.
Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza Koplo Jeremia akimpima kilevi kwa kutumia kifaa maalum dereva Nyange Migoko (katikati) wakati wa zoezi maalum la usalama barabarani lililofanyika katika kituo cha mabasi Nyegezi Mkoani humo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya "Wait to Send" inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanatumia vyombo hivyo. Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.