Maombi yako yamefanyika baraka katika kazi yangu hii mpya ambayo iko sokoni kwa sasa inayoenda kwa jina la NIPE NGUVU YA KUSHINDA. Nimemuona Mungu akinipa Nguvu za kushinda katika maisha yangu, hata ninapopitia magumu lakini Mungu huyu ninayemwamini kila siku ananishindia.
Ningependa kukutia moyo rafiki yangu ya kuwa Mungu yupo na Mungu huyu huyu tunayemwabudu ni mwenye huruma na upendo. Unaweza ukaamuka asubuhi na usijue nini utaenda kukumbana nacho kazini kwako au mahali unapoenda, lakini ukashangaa Mungu anafungua milango ya kujipatia riziki yako. Una heri wewe unajipatia hata sh. 100 kwani kuna watu wengine hata hiyo unayopata hawapati.
Tuzidi kumtumikia Mungu kwani Mungu wetu wa huruma zana na ni mwema sana kwetu. Kukaa katika uwepo wake kuna faida sana kwani unakuwa umelindwa na malaika wa Bwana.
Nina mengi sana ya kuzungumza na wewe lakini kwa kupitia albamu yangu hii mpya, naamini Mungu atakuinua kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine. Ninachokuomba ni wewe kwenda kununua nakala hii na ukishanunua mwite na mwenzako mkae na kuisikiliza kwa makini na baada ya hapo chukua ho ujumbe na ufanyie kazi.
Mungu wangu na akubariki sana.