Wednesday, December 31, 2014

WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF WACHIMBA MTARO WA MAJI


WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF WACHIMBA MTARO WA MAJI
WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF WACHIMBA MTARO WA MAJI  KUPITIA UTARATIBU WA AJIRA YA MUDA KATIKA SHEHIA YA MPAPA,MKOA WA KUSINI UNGUJA.

Maelfu ya wakazi wa shehia ya Mpapa wilaya ya Kusini Unguja wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa maji unaotekelezwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaoratibiwa  na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa utaratibu wa ajira ya muda PWP.

Wakizungumza katika eneo la mradi baadhi ya walengwa hao wameonyesha utayari wao katika kuchimba mtaro huo huku wakiipongeza  serikali kupitia TASAF kwa kubuni utaratibu huo ambao wamesema licha ya kuwaongezea fedha lakini pia utapunguza kero ya upatikanaji wa maji katika eneo lao .

Chini ya utaratibu wa ajira za muda ,walengwa kutoka kaya maskini huibua miradi katika eneo lao na kuitekeleza na kisha kulipwa ujira ikiwa ni mkakati wa TASAF wa kuziongezea kaya maskini kipato kwa kukidhi mahitaji muhimu hususani katika Nyanja za elimu,afya,lishe na uchumi, ambapo kwa mujibu wa utaratibu asilimia  75 ya fedha ni malipo kwa walengwa wakati asilimia 25 ni kwa ajili ununuzi wa vifaa .

Mpango wa ajira za muda utatekelezwa nchini kote wakati wa kipindi cha hari au kipindi kigumu kama wakati wa ukame au mafuriko kupitia Mpango wa Kunusuru  kaya maskini,PSSN ambao umebuniwa na  serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na unatarajiwa kuhudumia kaya maskini zipatazo laki tisa na ishirini elfu nchini kote kazi ianayotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Marchi 2015.

ifuatazo ni picha za baadhi ya wananchi wa shehia ya Mpapa mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi ya kuchimba mtaro wa maji kupitia utaratibu wa ajira za muda.
 Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika shehia ya Mpapa mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi ya uchimbaji wa mtaro wa maji kupitia Mpango wa ajira za muda ambao huwawezesha walengwa kulipwa fedha .
 Mtaro wa maji uliochimbwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika shehia ya Mpapa wilaya ya Kusini Unguja inayotekelezwa chini ya mpango wa ajira za muda kupitia TASAF.

Mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini wa TASAF katika shehia ya Mpapa wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja akishiriki kazi ya kuchimba mtaro wa maji.