Wednesday, December 31, 2014

Msanii wa filamu bongo Irene Paul Atambulisha “PROJECT” yake, Asema Kila Mtu Nayake


Msanii wa filamu bongo Irene Paul Atambulisha "PROJECT" yake, Asema Kila Mtu Nayake
Mrembo na mwigizaji wa filamu hapa bongo, Irene Paul   "Angelina Jolie" wa bongo sababu wengi humfananisha na mwigizaji na mwongozaji nguli huyo wa filamu wa huko Marekani kwa muonekano wa sura hasa midomo ilivyojikata.
Tofauti na kwa mastaa wengi ambao huwa hawataki kuweka wazi "PROJECT" zao, Irene amekuwa muwazi zaidi baada ya kutupia picha hiyo matandaoni na kuaandika maneno yanayoashilia kuwa huyo jamaa ambae alim-TAG kwa jina la Duma wapo kwenye mahusiano.
Irene aliandika maneno haya kwa kifupi "kila mtu na project"
Kwananeo hayo tu mashabiki wake walianza kumpongeza kwa uwazi wake  na kumtakia kila la kheri kwenye mahusiano hayo huku irene akionysha kuzipokea pongezi hizo na dua za mashabi wake.
Nasi pia tunamtakia kila la kheri na project iendelee.