Baadhi ya watu mashuhuri waliotunukiwa Nishani na Rais Jakaya Kikwete.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), Rais mstaafu Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakiwa katika hafla ya kutunuku Nishani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akimvisha Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili na Rais Jakaya Kikwete, Pius Chipanda Msekwa.
Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Pius Chipanda Msekwa baada ya kumtunuku Nishani.
Rais Jakaya Kikwete akimvisha Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili Samuel John Sitta.
Jaji Augustino Ramadhani akivishwa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili na Rais Jakaya Kikwete.
Jaji Augustino Ramadhani akivishwa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili na Rais Jakaya Kikwete.
Paul Milyango Rupia akivishwa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili.
Anna Abdallah akipokea Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu.
Kingunge Ngombale Mwiru akipokea Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu.
Mwakilish wa marehemu Isaack Abraham Sepetu akipokea Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.
Ali Ameir Mohamed akivishwa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu na Rais Jakaya Kikwete.
Balozi Augustine Mahige akivishwa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu.
IGP mstaafu, Phillemon Mgaya akipata Nishani na Tuzo kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu.
Bibi Johari Yusuf Akida akipata Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Nne.
Mwakilishi wa Band ya Atomic Jazz Band akipata Nishani Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Nne.
Rais Jakaya Kikwete akimvisha Nishani ya Ushupavu Kassim Said Kassim ambaye ni muuza Chips katika maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam, Kassim alitunukiwa Nishani hiyo baada ya kupambana na jambazi aliyevamina na kupora wateja katika eneo la biashara yake na kumpiga chepe na kusababisha kupatikana kwa bastola moja pamoja na risasi tano.
Brass Band ikitumbuiza katika hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na wawakilishi wa watunukiwa wa Nishani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waliopata Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete.
Waliopata Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete.
Rais akiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi wa marehemu Sophia Kawawa pamoja na Bibi Johari Yusuf Akida (kulia) baada ya kuwatunuku Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Nne.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi wa marehemu Brigedia Jenerali mstaafu Adam Mwakanjuki (kulia)
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mtunukiwa wa Nishani ya Ushupavu, Kassim S Kassim wa pili kulia.
Hongera kwa ushupavu uliouonyesha......
Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Kassim Said Kassim baada ya kumtunuku Nishani ya Ushupavu.