Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan JICA, Kato Hiroshi akimueleza jambo Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo Sekta ya Ujenzi wa barabara nchini wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa JICA Kato Hiroshi.
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Gerson Lwenge ( wapili kulia), akimuuliza swali Makamu wa Rais wa JICA Kato Hiroshi (wa kwanza kushoto) kuhusu miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Shirika hilo la Maendeleo.
Baadhi ya wajumbe kutoka JICA wakiangalia baadhi ya picha za matukio mbalimbali katika Wizara ya Ujenzi kabla ya mkutano wao na Waziri wa Ujenzi.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa JICA, Kato Hiroshi mara baada ya kumaliza mkutano wao uliofanyika Wizara ya Ujenzi.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI.