Tuesday, December 30, 2014

kakakuona aonekana kigamboni leo, wananchi watabiri ni ishara ya mvua nyingi msimu huu


kakakuona aonekana kigamboni leo, wananchi watabiri ni ishara ya mvua nyingi msimu huu
 Wananchi wakiwa wamemzunguka Kakakuona aliyeonekana asubuhi majira ya saa moja maeneo ya Kigamboni Kisiwani Mtaa wa Chaboko ambapo kwa mujibu wa ripota na mpiga picha wetu Salma Bob Kassim, mnyama huyo aliwekewa Unga, ndizi, maji pamoja na pesa. 
Lakini akaishia kunywa maji tu kabla ya kukimbilia vichakani. Wananchi kwa mamia waliofurika kumuona Kakakuona huyo walisikika wakisema kuwa huenda huo ni utabiri kwamba huenda mvua zikawa nyingi msimu huu. 
Polisi walifika eneo la tukio na baada ya kuona hakuna uvunjifu wa amani wakatoa taarifa kwa maafisa wa Maliasili ambao walifika na kumtia mnyama huyo kwenye kiroba na kuondoka naye
 Kakakuona akijikunja baada ya umati wa watu kuzidi kuwa mkubwa 
Baadaye, huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha, Kakakuona huyo alielekea vichakani huku umati ukiendelea kumshangaa. Baadaye watumishi wa Maliasiali walifika na kumtia kwenye kiroba na kuondoka naye.
Picha na Salma Bob Kassim