Sunday, December 07, 2014

Dkt Shein aongoza maziko ya Muasisi wa CCM Marehemu Mzee Juma Ameir Juma



Dkt Shein aongoza maziko ya Muasisi wa CCM Marehemu Mzee Juma Ameir Juma
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) akijumuika na  waislamu na Viongozi kumuombea dua  Muasisi wa CCM  Marehemu Mzee Juma Ameir Juma baada ya kumswalia katika Msikiti wa Abdalla Rashid Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi na amezikwa leo kijijini kwao  Muungoni Wilaya ya Kusini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi AlhajDk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) pamoja na Viongozi na Waislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Muasisi wa CCM  Marehemu Mzee Juma Ameir Juma  baada ya kumswalia katika Msikiti wa Abdalla Rashid Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi  na kwenda kuzikwa leo kijiji kwao Muungoni Wilaya ya Kusini Unguja
 Wananchi wakilibeba jeneza lenye mwili wa marehemu muasisi wa CCM marehemu Mzee Juma Ameir Juma aliyefariki leo na kuzikwa  kijijini kwao Muungoni  Mkoa wa Kusini Unguja,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  aliongoza maziko hayo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi (katikati) pamoja na Waislamu na Wananchi mbali mbali wakishiriki katika Maziko ya muasisi wa CCM  Marehemu Mzee Juma Ameir  Juma aliyefariki usiku wa kuamkia leo na kuzikwa  kijijini kwao Muungoni wilaya ya Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitia udongo katika kaburi la muasisi wa CCM  Marehemu Mzee Juma Ameir  Juma aliyefariki usiku wa kuamkia leo na kuzikwa  kijijini kwao Muungoni wilaya ya Kusini Unguja.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuaiakitia udongo katika kaburi la muasisi wa CCM  Marehemu Mzee Juma Ameir  Juma aliyefariki usiku wa kuamkia leo na kuzikwa  kijijini kwao Muungoni wilaya ya Kusini Unguja.
Mjumbe wa Baraza la Wazee wa CCM Haji Machano akisoma wasifu wa muasisi wa CCM  Marehemu Mzee Juma Ameir  Juma baada ya mazishi yake yaliyofanyika leo kijijini kwao Muungoni wilaya ya Kusini Unguja mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein. Picha IKULU, Zanzibar