Sunday, December 07, 2014

MOSHI VETERANI WAMKUMBUKA MUASISI WAO MAREHEMU MADESHO MOYE



MOSHI VETERANI WAMKUMBUKA MUASISI WAO MAREHEMU MADESHO MOYE
Marehemu Madesho Moye wa pili kutoka kulia (waliopiga magoti)akiwa na kikosi cha timu ya soka ya Moshi veterani ya mkoani Kilimanjaro kilipofanya ziara nchini Kenya April Mwaka huu katika mashindano ya kombe la Pasaka ambalo timu hiyo ilifanikiwa kunyakua.
Marehemu Madesho Moye(wakati wa uhai wake) akiwa amebeba kombe baada ya kufanikiwa kushinda kikombe
hicho katika mashindano ya Pasaka ambayo huandaliwa kila mwaka na mamlaka  ya bandali ya nchini Kenya.
Marehemu Madesho Moye(wakati wa uhai wake) akiwa amebeba kikombe mara baada ya kukabidhiwa baada ya kuwa washindi katika mashindano ya Pasaka yaliyofanyika nchini Kenya
Watoto wa Marehemu Madesho Moye wakiongozwa na, Raymond Madesho(katikati) mchezaji wa timu ya Panone FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza wakiweka shada la maua katika kaburi la Baba yao.
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya jamii Kanda ya kaskazini.