Wednesday, November 12, 2014

MAKAMU WA RAIS, MAKINDA, WAMZIKA RAIS SATTA WA ZAMBIA



Spika wa Bunge la Zambia Mhe. Jaji Patrick Matibini akimwelekeza jambo Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda wakati wa Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata aliyezikwa jana mjini Lusaka
Wanajeshi wakilisindikiza gari maalum lililouchukua mwili wa hayati Michael Satta, wakati ukiwasili uwanja wa soka mjini Lusaka, kwenye ibada ya misa ya mazishi ya kiongozi huyo jana Jumanne
Makamu wa rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe(Wapili kulia), wakitoa heshima mbele ya kaburi la marehemu Satta, baada ya kuweka mashada ya mauza wakati wa mazishi ya kiongozi huyo
Rais wa bunge la SADC, na spika wa bunge la Tanzania, Anne Makinda, akitoa heshima baada ya kuweka shada la mauza kwenye kaburi la hayati rais Satta
Wanajeshi wakishusha jeneza lenye mwili wa Satta kaburini, wakati wa mazishi yake
Makamu wa rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (Wakwanza kushoto0, rais mstaafu wa Namibia, Sam Nujoma, (Wapili kushoto), rais mstaafu wa Zambia Rupia Banda, (Watatu kushoto) na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, wakifuatilia misa wakati wa mzishi ya rais wa Zambia, Michael Satta jijini Lusaka Zambia Jumanne Novemba 11, 2014
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Mhe. Nkosazana Dlamini Zuma wakati wa Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata mjini Lusaka jana. aliyeketi ni Spika wa Bunge la Zambia Mhe. Jaji Patrick Matibini