Saturday, October 04, 2014

Wizara ya uchukuzi yasaini mkataba na kutekeleza amradi wa treni za kisasa nchini



Wizara ya uchukuzi yasaini mkataba na kutekeleza amradi wa treni za kisasa nchini
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Kipalo Kisamfu(aliyevaa koti la kaki), na Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Marekani na mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja kutoka nchini Marekani, Robert Shumake wakisaini Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo asubuhi katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi. Wanaoshuhudia na Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe (wan ne kutoka kulia), na wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka ( wa tatu kutoka kushoto) pamoja na wawakilishi kutoka kwa Mwanansheria Mkuu wa Serikali, Mwenyekiti wa Bodi ya TRL.
Balozi wa heshima wa Tanzania Nchini Marekani na mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja , Robert Shumake, akiwaelezea waandishi wa habari(hawapo pichani), namna treni ya mwendo kasi itakavyotengezwa baada ya utiaji saini wa Mkataba wa maelewano wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo asubuhi katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) , akisisitiza jambo wakati akiongea na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani na na mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja, Robert Shumake, ofisini kwake kabla ya kusaini Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zijulikanazo kama Diesel Multiple Unit(DMU) zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (mwenye tai nyekundu), akisisitiza jambo kabla ya utiaji saini Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo asubuhi katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi.
Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Marekani na mfanyabiashara nchini Marekani na mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja, Robert Shumake akimueleza Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi, Wizara ya Uchukuzi, Peter Lupatu namna treni ya mwendo kasi itakavyofanya kazi, kabla ya utiaji saini wa Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi. Treni hiyo itabeba abiria 800 mpaka 1000. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)