Tuesday, December 30, 2014

Waziri Mwandosya akagua Miradi ya Umwagiliaji ,Busokelo, Rungwe



Waziri Mwandosya akagua Miradi ya Umwagiliaji ,Busokelo, Rungwe
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya (wa pili kulia) akipata maelezo ya Mradi wa Umwagiliaji wa Mbaka.Utakapo kamilika Mradi utakuwa na uwezo wa kumwagilia hekta 600 kwenye vijiji vya Mbambo,Kambasegele,Katela,na Kapula-Mpunguti.Wananchi 1300 watanufaika na Skimu hii.wengine pichani kutoka kulia ni Gideon Mapunda,Afisa Kilimo,Ndugu Said Mzeru,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busokelo na Mhe. Alfred Mwakasapi,Diwani wa Kata ya Kambasegela;wakiwa kwenye banio la chanzo cha mradi kwenye Mto Mambwe.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya (wa pili kushoto) akipata maelezo ya utekeelezaji wa miradi ya umwagiliaji Busokelo kutoka kwa Afisa Umwagiliaji wa Halmashauri,Ssid Majula,wa nne kushoto.
Waziri Mwandosya akagua mfereji mkuu wa skimu ya umwahgiliaji ya Mbaka.