Tuesday, December 30, 2014

THE MBONI SHOW KUANZA KUUNGURUMA JANUARY 2 NDANI YA TBC


Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba (wa pili ktoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana katika  ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kuanza kwa msimu wa tatu wa kipindi chake 'The Mboni Show' kinachotarajia kuanza Jan 2, 2015. Kushoto ni kiti MC Zimpompa na kuanzia kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba.
Kutoka Kulia Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema akizungumza wakati wa uzinduzi kipindi cha Mboni Show uliofanyika katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba pamoja na Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba.

Na Mwandishi Wetu.
Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba ameamua kuhamishia kipindi cha Mboni show katika kituo cha utangazaji cha Taifa (TBC) kutoka EATV ili kuvutia watazamaji wengi na wapya kwa wazee pamoja na vijana.
Kipindi cha Mboni Show kitaanza kurushwa TBC kuanzia January 2 mwaka 2015 siku ya
Ijumaa saa 3 Usiku-4 Usiku na marudio Jumanne saa 9:00 mchana-10:00mchana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mboni Masimba ametoa shukrani kwa EATV kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote alichokuwa nao,na kusema kuwa amehamishia kipindi cha Mboni Show katika kituo cha TBC ili kuvutia watazamaji wengi na hakuna atakaye tumia jina la Mboni Show na hakuna kitakachomkwamisha kwa vile ana hati miliki.
"Nimehamia TBC kwa kuwa nahitaji watazamaji wengi ,wote wazee na vijana na hakuna atakaye tumia jina langu la Mboni Show kwa kuwa nina hati miliki ya jina hili", alisema Mboni.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw.Fadhili Chilumba amesema wamefurahi kuwepo kwa Mboni Show katika kituo cha Taifa(TBC) na kutoa wito kwa mashabiki kuweza kuwadhamini watu kama wakina Mboni na wanamkaribisha sana.
Nao wadhamini wa Mboni Show,Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema wamesema wanamwezesha Mboni kuwepo hewani ili kuhamasisha,kuelimisha pamoja na kuburudisha umma wa Watanzania.