Sunday, October 12, 2014

Waziri Membe Aongoza Matembezi ya Hisani Dar es Salaam



Waziri Membe Aongoza Matembezi ya Hisani Dar es Salaam
Matembezi ya hisani yaliyoanzia Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe Mwenge yakielekea Parokia ya Sinza kupitia barabara ya Shekilango. Matembezi hayo ya kilomita mbili yaliongozwa na Mhe. Membe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.) (wa pili kushoto mstari wa mbele) akishiriki matembezi ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokovu ya Kanisa Katoliki Sinza, Dar es Salaam mapema leo asubuhi..Wa kwanza kushoto ni  Paroko, Father  Cuthbert Maganga Sasagu, na wa tatu kushoto ni  Mwenyekiti wa Parokia hiyo, Bw. Arnold Mwasumbi.
Waziri Membe akizungumza na waamini wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokovu Sinza.
Baadhi ya waamini wa parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokovu Sinza wakimsikiliza Waziri Membe .
Waziri Membe akipokea Zawadi ya picha kutoka kwa Paroko Sasagu
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na viongowa wa parokia ya Sinza.
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na wapuliza Tarumbeta.