Sunday, October 12, 2014

ZIARA YA KIKAZI YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS - MAZINGIRA KATIKA KANDA YA ZIWA


ZIARA YA KIKAZI YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS - MAZINGIRA KATIKA KANDA YA ZIWA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Dkt. Binillith S.Mahenge akipewa maelezo na Mratibu wa NEMC kanda ya Ziwa Bi. Anna Masasi kuhusu uharibifu wa Mazingira ya Mwambao wa Ziwa Viktoria katika eneo la Nera, unaosababishwa na shughuli za Kilimo na ufugaji wa samaki katika eneo hilo jijini Mwanza.
Sehemu ya mwambao wa Ziwa Viktoria katika eneo la Nera jijini Mwanza likionesha shughuli za kilimo zinazofanyika katika eneo hilo na kusababisha uharibifu wa mazingira akioneshwa jinsi taka za plastiki zinavyochakatwa kutwnwza bi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa magugu maji kunakosababishwa na mbolea inayotumika katika shughuli za kilimo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Dkt. Binillith S.Mahenge akioneshwa jinsi taka za plastiki zinavyochakatwa kutengeneza bidhaa mbalimbali, kama vile Mifuko ya Plastiki, alipotembelea kiwanda cha Falcon Parkaging Ltd cha jijini Mwanza. Anayetoa maelezo ni Mkurugenzi wa Kiwanda Bwana Ganeshan Vedagiri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Dkt. Binillith S.Mahenge akioneshwa mbao iliyengezwa kutokana na taka za plastiki katika kiwanda cha Falcon Packaging Ltd cha jijini Mwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Dkt. Binillith S.Mahenge akioneshwa mifuko ya plastiki inayotengenezwa na kiwanda cha Falcon Packaging Ltd kutokana na taka za plastiki zinazokusanywa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Mwanza.