Thursday, October 09, 2014

Taarifa ya Kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Muhidini Mfaume Kimario


Taarifa ya Kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Muhidini Mfaume Kimario
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepokea mwili wa Marehemu Meja Jenerali Muhidini Mfaume Kimario (Mstaafu) kutoka nchini India leo tarehe  09 Oktoba, 2014 katika uwanja wa Kimataifa wa Mwl JK Nyerere Dar es salaam,mwili wa marehemu umewasili kwa Shirika la ndege la Ethiopia saa 7:30 mchana.  

Mwili wa marehemu utaagwa kesho tarehe 10 Oktoba, 2014 saa 4:00 asubuhi katika viwanja vya hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na baadaye mwili utasafirishwa kwenda kwao Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika tarehe 11 Oktoba, 2014 saa 7:00 mchana siku ya Jumamosi.              

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh.  Dkt Hussein Mwinyi anatarajiwa kuongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
MEJA JENERALI MUHIDINI KIMARIO (MSTAAFU)
AMINA

Imetolewa  na:

Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, 
Upanga

S.L.P  9203,   
Dar es Salaam,  
Tanzania.