Waziri wa Mambo ya Ndani                ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,                Mathias Chikawe (kushoto) akizionesha kadi za Chama Cha                Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kukabidhiwa na                Katibu wa Kata ya Lionja, Wilayani Nachingwea, Hashimu                Halifa (kulia). Waliorudisha kadi hizo na kujiunga na CCM                ni Lusia Mohammed, Abdu Ngawina na Mohammed Kindamba.                Waziri Chikawe ambaye yupo katika ziara ya kikazi jimboni                kwake aliwaomba Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM                Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee                katika Kata hiyo kuhakikisha chama kinaimarishwa zaidi na                kuwakaribisha wanachama wote wanaotoka vyama vingine ili                wajiunge na CCM. 
                Waziri wa Mambo ya Ndani                ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,                Mathias Chikawe akizungumza na Wajumbe wa Mabaraza ya                Jumuiya zote za CCM Kata ya Lionja, Viongozi wa Dini na                Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo, Wilaya ya                Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe ambaye yupo katika                ziara ya kikazi katika Jimbo lake la Nachingwea aliwaomba                wajumbe hao kuhakikisha chama kinaimarishwa zaidi na                kuwakaribisha wanachama wote wanaotoka vyama vingine ili                wajiunge na CCM. 
                Waziri wa Mambo ya Ndani                ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,                Mathias Chikawe (kulia) akizungumza na Mjumbe wa CCM Kata                ya Lionja ambaye ni mlemavu wa miguu, Hassan Chingwale                baada ya kumaliza kikao chake na Wajumbe wa Mabaraza ya                Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa                Baraza la Wazee katika Kata hiyo, Wilaya ya Nachingwea                mkoani Lindi. Waziri Chikawe yupo katika ziara ya kikazi                jimboni mwake, aliwaomba wajumbe hao kuhakikisha chama                kinaimarishwa zaidi na kuwakaribisha wanachama wote                wanaotoka vyama vingine ili wajiunge na CCM. Picha na zote                na Felix Mwagara. 
        


 
