Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Ramadhan Mwinyi akichangia majadiliano kuhusu ajenda ya uthibiti wa silaha za nyukilia hapo siku ya jumanne. Akizungumza msimamo wa Tanzania kuhusu silaha hizo, Balozi Mwinyi amezitaka nchi zinazomiliki silaha hizo kuonyesha utashi wa kisiasa wa kuzipunguza na kuzidhibiti ili zisisambae kiholela lakini pia waihakikishie dunia usalama wake.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wakifuatilia majadiliano kuhusu upunguzaji wa silaha za nyukilia ambapo wazungumzaji wengi pamoja na Tanzania walisisitiza haja na umuhimu wa kuwa na maeneo huru yasiyo na silaha za nyukilia kwa usalama wa dun dunia na wakatoa wito kwa Shirika linalohusika na masuala ya Nguvu za Nyukilia kuhakikisha kwamba kila nchi inakuwa na haki ya kupata elimu na teknolojia inayohusiana na nguvu za nyukilia bila ubaguzi au upendeleo.