Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati (wapili kushoto) na Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) wakimsikiliza kwa makini Meneja wa kitengo cha mafuta cha Kurasini Oil Jet (KOJ), Capt. Mwingamno wakati Dk. Sri Mulyani Indrawati alipokitembelea kitengo hicho kilichopo ndani ya bandari ya Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati (katikati) na mwenyeji wake Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumzia jambo na Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadh Massawe wakati alipoitembelea bandari hiyo hivi karibuni.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Aloyce Matei akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati (hayupo pichani) wakati alipoitembelea bandari hiyo hivi karibuni.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la DFID nchini Tanzania Bibi Ros Cooper akizungumza jambo wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati alipoitembelea bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.
Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaabaan Mwinjaka, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la DFID nchini Tanzania Bibi Ros Cooper, Afisa Mtendaji Mkuu wa TradeMark East Africa (TMEA), Bw. Frank Matsaert na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Philippe Dongier wakisaini makubaliano maalumu (MoU) na TPA ya kuendeleza miradi mbalimbali maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam. Makubaliano hayo yalisainiwa mbele ya Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati na Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe akikabidhi zawadi ya kuutangaza utalii wa Tanzania kwa Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati wakati alipoitembelea Bandari ya Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati (wapili kulia) na Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadh Massawe akifafanua jambo wakati Dk. Sri Mulyani Indrawati alipoitembelea bandari hiyo hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati (wapili kulia) na Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mashirika ya Kimataifa, Wizara na TPA.Picha kwa hisani ya: Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)