Na Editha Karlo, Kigoma
ZAIDI ya Tani 24 za vyakula,dawa za binaadam na vipodozi zimeteketezwa na mamlaka ya chakula na dawa(TFDA)katika mikoa minne ya kanda ya katikwasababu ya kutofaa kwa matumizi ya binaadam.
Akizungumza wakati wa zoezi la uteketezaji wa bidhaa hizo zilizokamatwa katika zoezi la kustukiza ndani ya Manispaa ya Kigoma ujiji Mkoani hapa Mkaguzi wa TFDA kanda ya kati Engliber Bilashoboka alisema kuwa bidhaa hizo zilikamatwa kati ya Julai mwaka jana na Juni mwaka huu.
Bilashoka alisema kuwa kuteketezwa kwa bidhaa hizo kunatokana na ukaguzi unaofanywa na maofisa wa TFDA katika mikoa mbalimbali nchini na lengo likiwa ni kuondoa sokoni bidhaa zilizoisha muda wake na zisizofaa kwa matumizi ya bindaadam
Alisema pia kufuatia zoezi hilo mamlaka yake imekifungia kiwanda cha mikate cha Kigoma bekari baada ya kukutwa na tani 1.5 za mikate mibovu, pamoja na machinjio ya ujiji kwa kufanya shughuli zake katika hali inayotishia afya za wananchi
Alisema bidhaa hizo zimekamatwa katika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na dodoma alisema kuwa katika bidhaa zilikamatwa na kuteketezwa nyingi zilikuwa zikiuzwa huku muda wake wa kuwa sokoni ukiwa umeisha na zingine zimepigwa marufuku kuuzwa nchini. Ofisa huyo alisema kuwa uteketezaji katika manispaa ya kigoma kwa muda wa wiki moja mpaka sasa ,alisema mamlaka ya ke imeteketeza zaidi ya tani 4.1zenye thamani ya shilingi milioni 24 ambavyo havifai kwa matumizi ya binaadamu Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Moses Welansari akizungumzia zoezi hilo alisema kuwa wamekuwa wakikutana changamoto za wenye maduka zilizokatazwa au zilizoisha muda wake wa matumizi.
''Elimu imekuwa ikitolewa kwa wafanyabiasha mara kwa mara ili kuepuka kuweka sokoni bidhaa zisizotakiwa na mamlaka za serikali na zilizoisha muda wake ''alisema Kaimu Mkurugenzi
Shehena tani 1.5 ya mikate mibovu kutoka Kigoma Bakery ikishushwa kwenye dampo la Businde Mkoani Kigoma tayari kwa kuteketezwa kutokana na kutofaa kwa matumizi ya binadam shehena hiyo imebambwa kufuatia msako wa kushitukiza wa (Mamlaka ya chakula na dawaTFDA)
Zaidi ya tani moja na nusu za dawa binadaam kutoka duka la Mambo Leo la mjini kigoma zimeteketezwa na TFDA baada ya kuonekana hazifai kwa matumizi ya bindaadam
Bidhaa mbalimbali za madukani zikiwa tayari kwaaajili ya kuteketezwa baada ya muda wake wa matumizi kuisha,kufuatia msako wa kushitukiza wa TFDA