Waimbaji watatu wa muziki wa injili nchini Rose Muhando, Christina Shusho pamoja na mwimbaji wa muziki wa kufokafoka ama rap za injili Gazuko Junior wanapigiwa kura kwasasa pamoja na waimbaji wengine wa bara la Afrika ili kumpata mmoja wao atakayeshinda tuzo za Africa gospel music awards 2014 katika vipengele tofauti, tuzo zinazotarajiwa kutolewa mapema wiki ijayo jijini London nchini Uingereza.
Rose Muhando anawania tuzo ya mwimbaji wa kike wa mwaka Female artiste of the year ikiwa ni mara yake ya kwanza kuwemo katika tuzo hizo. Yeye anawania tuzo na waimbaji wengine maarufu Afrika akiwemo Ntokozo Mbambo, Vicky Vilakazi, Diana Hamilton, Winnie Mashaba, Gloria Muliro pamoja na Sarah K wote wa Kenya pamoja na waimbaji wengine ikiwa jumla ya waimbaji 15. Kikubwa ni kumpigia kura ROSE MUHANDO katika kipengele hiki.
Kwa upande wa Christina Shusho ambaye alichukua tuzo ya mwimbaji bora wa mwaka 2013 kwa Afrika Mashariki ameingia katika vipengele viwili mwaka huu. Kipengele cha kwanza kikiwa ni mwimbaji bora wa mwaka kwa Afrika mashariki Artiste of the year East Africa, mwaka huu akipambana na waimbaji kama Eunice Njeri, Sarah K, Gloria Muliro, Solomon Mukubwa ambaye katika tuzo hizo ametambulishwa kama Mtanzania, waimbaji wengine wa Kenya, Uganda pamoja na Ethiopia ikiwa jumla ya waimbaji 12. Kikubwa unapopiga kura tafuta jina la CHRISTINA SHUSHO na umpigie kura yako.
Aidha tuzo ya pili anayowania mwanamama Christina Shusho ni tuzo ya video bora ya mwaka Video of the year kupitia wimbo wake wa 'Nataka Nimjue' tuzo ambayo anawania na wanamuziki wengine kama Tehila Crew la Nigeria ambao pia mwaka jana waliondoka na tuzo, Daddy Owen wa Kenya, Sammie Okposo wa Nigeria na waimbaji wengine wanaofanya jumla ya waimbaji 15 wanaowania tuzo hizo. Kikubwa sie ni CHRISTINA SHUSHO wa kumpigia kura ingawa katika kipengele hiki kutakuwa na ushindani mkubwa hasa ikizingatiwa kwamba Afrika magharibi wanawapigia kura za kutosha waimbaji wao hata sisi tukijituma tunaweza.
Kwa mara ya kwanza katika historia mwanakaka Gazuko Junior kupitia uimbaji wake wa kufokafoka Afro Rap Artiste of the Year na waimbaji kutoka Uholanzi, Uingereza, Nigeria, Ghana, Malawi, Kenya, Botswana pamoja na Zambia. Kikubwa ni kumpigia kura GAZUKO JUNIOR ili tuzo ije Tanzania.
ama rap anawania tuzo ya mwimbaji bora wa rap wa mwaka
Ili kupiga kura BONYEZA HAPA
KUMBUKA ZIMEBAKI SIKU 3 TU KABLA ZOEZI LA UPIGAJI KURA KUFUNGWA. UNARUHUSIWA KUPIGA MARA NYINGI UWEZAVYO.