Mamlaka ya anga nchini India inachunguza tukio la hatari lililotokea Agosti 8, baada ya ndege ya Jet Airways Boeing 777-300 iliposhuka angani kwa zaidi ya futi 5000 (mita 1500) kutoka kwenye urefu waliopangiwa kuruka baada ya rubani wake kusinzia.
Tukio hilo lilitokea wakati ndege hiyo ikifanya safari kutoka Mumbai, India kwenda Brussels, Ubelgiji.
Times of India imeripoti kuwa rubani aliyekuwa akiongoza ndege hiyo alipumzika kidogo, mapumziko ambayo kwa viwango vya kimataifa huitwa 'controlled rest' kwa zile ndege za masafa marefu. Safari ya ndege kutoka Mumbai hadi Brussels ni masaa 9.
Rubani msaidizi alitakiwa kuchukua majukumu yote ya kuongoza ndege kwa wakati huo, lakini inadaiwa rubani huyo wa kike alisema naye alikuwa busy na tablet ya ndege hivyo hakugundua ndege ilipoanza kushuka kutoka kwenye urefu wa futi 34,000 iliyotakiwa kuruka wakati wanapita Uturuki.
Kwa bahati nzuri waongozaji wa anga wa Uturuki waligundua kuwa ndege hiyo iliyokuwa katika anga lao imeshuka kwenye urefu (altitude) ambao umepangwa kwaajili ya ndege nyingine, na kumtaarifu rubani msaidizi arudi kwenye urefu waliopangiwa.
Marubani wote wawili wa ndege hiyo wamesimamishwa kupisha uchunguzi .
Source: Aljazeera