Waziri Mkuu Mizengo Pinda                  akisisitiza jambo baada ya kupata maelezo juu ya                  maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni kabla ya                  kufanya ziara ya siku moja ya kutembelea Miradi                  iliyofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii                  (NSSF) jijini Dar es Salaam. 
                 Msimamizi wa Mradi wa ujenzi                  wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia)                  akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia)                  mchoro sanifu wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya                  waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa  inayofadhiliwa                  na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar                  es Salaam. 
                 Msimamizi wa Mradi wa ujenzi                  wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia)                  akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia)                  hatua za ujenzi wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara                  ya waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa  inayofadhiliwa                  na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar                  es Salaam. 
                 Waziri Mkuu Mizengo Pinda                  (wapili kulia) akitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la                  Kigamboni unaofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya                  Jamii (NSSF) wakati wa ziara yake ya siku kutembelea                  miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar                  es Salaam Jumamosi.
                 Waziri Mkuu Mizengo Pinda                  (Watano Kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya                  viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa                  Hifadhi ya Jamii (NSSF) mara baada ya kutembelea mradi                  wa daraja la Kigamboni ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya                  siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa                  inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi. 
                 Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa                Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akitoa                maelezo juu ya mradi wa NSSF wa nyumba wa Mtoni Kijichi                wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, kwa waziri mkuu                Mizengo Pinda (wapili kushoto) wakati wa ziara yake ya                siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa                inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
        Meneja Miradi wa Mfuko wa                  Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo                  akitoa maelezo juu ya mradi wa NSSF wa nyumba wa Mtoni                  Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, kwa                  waziri mkuu Mizengo Pinda (kulia kwake) wakati wa ziara                  yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa                  inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
                  Meneja Miradi wa Mfuko wa                  Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo                  (wa kwanza kushoto mbele) akitoa maelezo juu ya mradi wa                  NSSF wa nyumba wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya                  shilingi bilioni 4,500, kwa waziri mkuu Mizengo Pinda                  (wapili kushoto mbele) wakati wa ziara yake ya siku moja                  ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na                  NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
                 Meneja Miradi wa Mfuko wa                  Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo                  (kushoto) akimuonyesha waziri mkuu Mizengo Pinda (wapili                  kulia) moja ya sehemu za ndani ya mradi wa nyumba wa                  NSSF wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni                  4,500, unaondelea kujengwa, wakati wa ziara yake ya siku                  moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofsdhiliwa                  na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.        
         Waziri Mkuu Mizengo Pinda                  (watano kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya                  viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa                  Hifadhi ya Jamii (NSSF) mara baada ya kutembelea mradi                  wa nyumba za NSSF wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya                  shilingi bilioni 4,500 wa nyumba zenye gharama nafuu,                  ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea                  miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar                  es Salaam Jumamosi. 
                 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa                  Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadani Dau                  (kushoto) akitoa maelezo juu ya miradi ujenzi wa kijiji                  cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village modern city                  Housing scheme' yenye thamani ya matrilioni. Waziri Mkuu                  Mizengo Pinda alikuwa na ziara ya siku moja ya                  kutembelea miradi mikubwa ya miundombinu ya mfuko huo                  jijini Dar es Salaam.
                Waziri                  Mkuu Mizengo Pinda (Wapili kulia) akipata maelezo juu ya                  jinsi mabomba ya plastiki yanatengenezwa, wakati wa                  ziara yake alipotembelea mradi wa Ujenzi wa kijiji cha                  kisasa unaoitwa 'Dege Eco Village modern city Housing                  scheme' Jumamosi jioni. Mradi huo wenye thamani ya dola                  za kimarekani  544, 530, 562 unafadhiliwa                  na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa                  asilimia 45 ya hisa na Azimio Housing Estates Co. Ltd                  kwa asilimia 55 ya hisa. 
                Waziri                  Mkuu Mizengo Pinda (Wapili kulia) akipata maelezo juu ya                  jinsi mabomba ya plastiki yanatengenezwa, wakati wa                  ziara yake alipotembelea mradi wa Ujenzi wa kijiji cha                  kisasa unaoitwa 'Dege Eco Village modern city Housing                  scheme' Jumamosi jioni. Mradi huo wenye thamani ya dola                  za kimarekani  544, 530, 562 unafadhiliwa                  na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa                  asilimia 45 ya hisa na Azimio Housing Estates Co. Ltd                  kwa asilimia 55 ya hisa. 
         Serikali imesema itajipanga ili                kuona namna ya kukabiliana na changamoto mbali mbali                ambazo zitaweza kukwamisha miradi mikubwa yanayoendeshwa                na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) yatakayo                badilisha sura ya Jiji la Dar es Salaam..
        Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyasema                hayo baadaa ya kutembelea miradi mitatu mikubwa                inayoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)                amayo ni pamoja na daraja la Kigamboni, mradi wa nyumba za                gharama nafuu inayojengwa Mtoni Kijichi na mradi wa nyumba                Zaidi ya 7000 uitwao  'Dege Eco Village iliyopo Kigamboni.
        Akizungumza wakati wa kukamilisha                ziara yake huko Dege Kigamboni katika mradi wa nyumba                Zaidi ya 7000 uitwao  'Dege Eco Village' Jumamosi , Pinda                alisema Kigamboni inendelea kwa kasi kubwa kiasi kwamba                miundombinu iliyopo haitoshi kuhimili idadi ya watu                watakaohamia.
        "Tunahitaji kujipanga kwa dhati                kuhakikisha barabara na vivuko vinafanya kazi. Changamoto                kubwa hapa ni barabara za viuongo kutoka Mandela upande wa                Kurasini na upande wa Kigamboni pia. Barabara hivi zote                sita za darajani zitatakiwa kufika Kigamboni, Mjimwema,                Mbagala na kwingineko," alisema.
        Pinda alisema daraja litakapo                kamilika, watumiaji watatozawa tozo la barabara ili kuweza                kulihudumia. Alisema serilaki inafikiria pia namna ya                kuipanga Kigamboni ili iendane na maendeleo yanayokuja.
         Kuhusu Mradi mkubwa wa Dege Eco                Village wenye uwezo wa kuchukua nyumba za gorofa Zaidi ya                7000 na za kawaida (villas) 300, Waziri mkuu alisema mradi                huo utaleta msukumo mkubwa kwa maendeleo ya taifa kwani                hakuna mji utakao fanafana na ule kati ya miji mingi                aliyofika.
        Aliitaka Manispaa ya Temeke kuangalia                idadi ya watu kule Kigamboni  ili serikali iangalie                uwezekano wa namna ya kupanga usimamizi kiutawala.
        Pinda alifurahishwa na kitendo cha                NSSF kuwapa kipaumbele wanachama wake kupata nyumba ambazo                zimejengwa katika mradi wa Mfuko huo uliopo Mtoni Kijichi.                Tayari nyumba 85 zilizojengwa katika awamu ya kwanza                zimeshachukuliwa na wanachama. Ujenzi wa nyumba hizo                ulianza Novemba 2008 na kukamilika 2010.
        Nyumba 215 zilizojengwa katika awamu                ya pili nazo zimeshachukuliwa na wanachama na baadhi ya                wadau wengine. Nyumba hizo kwa mujibu wa Meneja Miradi,                Mhandisi John Msemo, zilianza kijengwa mwaka 2011 na                kumalizika mwaka 2013 ikiwa ni awamu ya tatu.
        Mhandisi Msemo alisema awamu ya tatu                ndio inaendelea kwa sasa ya ujenzi wa gorofa na nyumba za                kawaida (villas) jumla yake ikiwa ni nyuma 820, mradi                ambao ulianza mwaka jana 2013 na unatarajiwa kumalizika                2015. Tayari nyumba 300 zimeshalipiwa kabla                hazijamalizika.
        Akiongea na waandhishi wa habari baada                ya ziara ya waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, DK                Ramadhani Dau alisema miradi yao ilikuwa inapata                changamoto kubwa hasa upande wa barabara.
        "Tukimaliza ujenzi wa daraja                tunategemea barabara zote jijini ziwe zimeisha ili                kupunguza msongamano katika daraja. Itakuwa haina maana                kumaliza daraja wakati maungio hayajakamilika," alisema.
        Aliongeza pia kuwa kumekuwa na                changamoto mbalimbali katika kutekeleza wa miradi hiyo                ikiwemo ya kutopata ardhi toka kwa wananchi kwa muda                unaofaa, serikali kuchelewa kutoa asilimia 40 ya sehemu                yake katika mradi na pia masuala ya kitaalamu katika                ujenzi wa daraja.
        Kuhusu mradi wa nyuma Mtoni Kijichi,                alisema walikuwa wanahitaji sana daraja litakounganisha                Mtoni Kijichi na Mbagala kwani nirahisi sana kuvuka sehemu                hiyo na kuingia kigamboni kiurahisi kuliko kutumia Zaidi                ya kilometa 20 kuzunguka katika daraja ili mtu afike                Kigamboni au Mbagala.
        Tatizo la maji alisema walilazimika                kuchimba visima wakati DAWASA waki jiandaa kufanya                taratibu za kuweka maji.
        













 
