Sunday, August 17, 2014

MSIMU WA KOROSHO KUANZA AGOSTI 20, 2014



MSIMU WA KOROSHO KUANZA AGOSTI 20, 2014
Bodi ya korosho Nchini Imetangaza Kuanza rasmi kwa ununuzi na uuzaji wa korosho katika msimu wa 2014/2015 utakaonza tarehe 20 mwezi huu ili wakulima waweze kuitumia vema fursa ya kuvuna mapema korosho zao kabla ya nchi nyingine kuanza kuvuna. 
Mwenyekiti wa bodi ya korosho Tanzania Mhe Anna Abdallah (MB)ameyasema hayo akiongea na waandishi wa habari na kubainisha kuwa ili kufikia azima hiyo ya kutumia fusa ya uvunaji mapema ni vizuri wadau wote wanaohusika na uuzaji na ununuzi wakamilishe maandalizi muhimu kabla ya msimu kufunguliwa rasmi ili kuepuka ucheleweshaji wa ununuzi na uuzaji wa korosho msimu huu.
 Kufuatia kikao cha wadau wa tasnia ya zao la korosho katika mkutano wao mkuu wa mwaka uliofanyika mjini Masasi tarehe 9-10 mwezi huu wakulima walikubaliana kuwa bei dira(mwongozo)ya korosho ghafi daraja la kwanza kuuzwa na kuanzia tshs shilingi 1000/= kwa kila kilomoja.
Ambapo korosho daraja la pili zitauzwa na kununuliwa kwa shilingi 800/= kwa kila kilo moja ambapo alifafanua kuwa kuwa bei hizo ni za mwongozo tu kwani bei halisi itategemea nguvu ya soko ambapo inaweza kubadilika kutokana na Ushindani wa wanunuzi kupitia minada 
Aidha mwenyekiti huyo aliwataka wafanya biashara kujiandaa kufanya malipo ya leseni za biashara hiyo kufuatia miaka ya nyuma leseni za biashara zilikuwa zinatolewa bila malipo.
Hata hivyo kwa mujibu wa sheria ya fedha namba 5 ya mwaka 2011,kuanzia msimu huu leseni za ununuzi wa zao hilo zitatolewa kwa malipo Ambapo wanunuzi wa ndani watalipia ada ya shilingi 750,000/= na wanunuzi wa nje walipia ada ya dola za kimarekani 500/= kwa msimu Ununuzi wa zao hilo umekuwa ukiyumba katika baadhi ya misimu hasa kuhusiana na suala la bei kiasi cha kusababisha malalamiko na migogoro hata vurugu kutoka kwa wakulima dhidi ya serikali,vyama vya msingi na Ushirika 
Awali katika mkutano wa wadau wa korosho, BODI zote za mazao nchini zimetakiwa kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wakulima ili kuwajengea matumaini ya kuzalisha kwa wingi na kwa viwango vinavyohijtajika kwenye masoko ya ndani na nje na kuliletea taifa fedha za kigeni. Rai hiyo ilitolewa wilayani Masasi mkoani Mtwara na waziri wa kilimo,chakula na Injinia Christopher Chiza alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa wadau wa korosho Tanzania uliofanyika wilayani Masasi katika ukumbi wa Emirates  
Waziri Chiza Alisema kuwa bodi zote za mazao hapa nchini zinatakiwa zitatuwe matatizo ambayo wakulima wanakumbana nayo na kuwasababishia washindwe kufikia malengo yao waliyoyakusudia kunakotokana na viongozi wa bodi kukwepa kutimiza majukumu yao wanayotakiwa kuyatekeleza. "Kwa sasa kumekuwa na mwaya mkubwa kati ya bodi, Halmashauri za wilaya na miji,mifuko ya pembejeo na wakulima inayosababishia kutofanya vizuri na kumuacha mkulima akiwa kisiwani bila ya kupata msaada kupitia bodi hizo hivyo suala kubwa ambalo linapelekea kuwepo na mwanya huyo kunatokana na kutowashirikisha wakulima kwenye maamuzi mbalimbali ikiwemo kwenye kufanya mahesabu ya uendeshaji yanayohusu manunuzi,gharama za matumizi na malipo ya majaliwa ambayo ni kiini cha mafanikio kwa mkulima wa mazao.
"Wakulima wa Tanzania wako tayari kuzalisha bidhaa za mazao yao na Ili mkulima apewe matumaini ya kuzalisha mazao kwa tija bodi lazima ziwe mstari wa mbele katika utendaji wa majukumu yake kwa ufanisi na uaminifu zaidi na kutii sheria ya ushirika na kanuni zake kwakufanya hivi kutamsaidia mkulima,"alimalizia Waziri Chiza
Mwenyekiti wa bodi ya korosho Mhe Anna Abdallah  akifungua kikao cha wadau wa korosho kilichofanyika wilayani Masasi mkoani Mtwara kulia ni waziri wa kilimo na ushirika Injinia Christopher Chiza na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joseph Simbakalia. Kikao hicho kinajadili maendeleo na changamoto za zao hilo