Thursday, August 07, 2014

Kongamano la mchakato wa Katiba lasogezwa mbele


Kongamano la mchakato wa Katiba lasogezwa mbele
Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania limesema kwamba kongamano la kujadili chakato wa kutunga Katiba mpya na changamoto zake lililopangwa kufanyika Agosti 9 na 10  mwaka huu limesogezwa mbele, hivyo litatangaza tarehe ya kufanyika.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa  baraza hilo, Peter Mziray katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari mjini Dodoma leo.

"Kutokana na uzito wa kongamano hilo na kazi kubwa ya maandaliziyake, inayotokana na uwingi  na uzito wa wageni waalikwa, kongamano hilo halitafanyika siku ya tarehe 9 na 10 Agosti, mwaka 2014 kama lilivyopangwa awali. Hivyo basi  tarehe ya kufayika kongamano hilo imepelekwa mbele na baraza litatangaza," alisema Mziray.

 Aliongeza kuwa kongamano hilo litakuwa tukio kubwa na muhimu kwa nchini yetu, kwani litajadili kwa kina mchakato wa kutunga Katiba mpya unaoendelea  na changamoto zinazoendelea kukabiliana nazo.

" Wadau wote wanaohusika na mchakato huu wataalikwa na watoa maoni yao," alisisitiza.
 Aidha Mziray alisema kongamano hili litaibuka na maazimio ambayo, baraza hilo, linaamini yatakuwa na uzito na ushawishi  katika mchakato huo kwa kuwa yatazingatia maslahi mapana ya taifa, hali  halisi ya siasa, uchumi, utamaduni, jamii na haja ya kudumisha Muungano wetu na hatima ya nchi kwa miaka mingi inayokuja.

Awali akizungumza na waandishiwa habari hivi karibuni jijini Dares Salaam kufuatia kufanyika  Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa baraza hilo, Peter  Kuga  Mziray, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao kati ya baraza hilo, na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa,akiwemo Msajili  wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi kilichofanyika kwenye hoteli ya New Afrika jijini Dares Salaam.

Mwenyekiti huyo akizungumzia kuhusu kongamano hilo ,ambalo litamhusisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya  Kikwete,ambaye atakayelifungua, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe . Mohammed Gharib Bilal, Marais wastaafu,wabunge,majaji, maspika, viongozi wote waliowahi kushika madaraka, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini zote.

"Lengo la kongamano hili ni kujadili hali ya kisiasa na mchakato wa Katiba Mpya. Kongamano hili ndio njia ya kutafuta maridhiano  katika suala hili. Tunategemea busara za viongozi hawa zitatubadilkisha  na kutuweka pamoja  kwa maslahi ya taifa na kuachana na mambo ya kivyama," alisisitiza.