Sunday, July 27, 2014

Salam kwa Wana DMV toka kwa Harriet Shangarai



Salam kwa Wana DMV toka kwa Harriet Shangarai
Ndugu zangu wanaDMV, nilikuja kwenu rasmi nikiomba kura zenu.Nia yangu ikiwa ni kuungana nanyi katika kutafuta njia za kutatua changamoto zinazotukabili hapa ugenini.

Malengo niliyo nayo kwa jumuiya hii na kwa jamii kwa ujumla sio malengo ya mpito.

Sisi wanaDiaspora tumeaacha nchi yetu nzuri, wazazi,watoto, ndugu hata marafiki kwa nia ya kuja kutafuta ahueni ya maisha.Maumivu na changamoto za ugenini ni sababu tosha za kutoruhusu jambo lolote kupotosha malengo yetu.

Nipo pamoja nanyi kama mgombea asiyefungamana na upande wowote, na nitaendelea kuwa nanyi licha ya matokeo ya Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya WaTanzania, District of Columbia, Maryland and Virginia 2014.

Asanteni sana.
Harriet Shangarai