BARABARA YAANGUKA NCHINI BRAZIL KWENYE MJI MWENYEJI WA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA
Barabara hiyo ipo kilometa 3 kutoka Mineirao Stadium,uwanja uliotumika kwa mechi mbali mbali za kombe la dunia na utatumika kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014.
Barabara hii ilikuwa ni moja ya kiungo kinachounganisha uwanja wa mpira na uwanja wa Kimataifa wa Ndege. Barabara hiyo ni mpango wa mbasi ya mwendo kasi ambayo ilisemekana ingekuwa tayari kutoa huduma wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia.